Bepari Classic: Burudani
Breaking News
Loading...
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Burudani. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Burudani. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 28 Oktoba 2016

Alikiba aelezea ujio wa single mpya aliyoshirikishwa na Ommy Dimpoz

Ni October 28, 2016 ambapo mkali kutoka Bongo Flevani, Alikiba amefunguka na kuweka wazi ujio wa single mpya aliyoshirikishwa na Ommy Dimpoz iitwayo Kajiandae.

Staa huyo akizungumza kwenye kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa kupitia Clouds TV aliyaongea haya>>>>Kiukweli kwanza ni wimbo mzuri pili maandalizi ya video hiyo tayari tumeshafanya na jina la wimbo unaitwa Kajiandae kwahiyo mashabiki wangu na mashabiki wa Ommy Dimpoz wakati wowote watapata ladha nzuri tu kwani najua ni kitu gani mashabiki wa muziki wangu wanachokitaka kutoka kwangu’

Jumapili, 16 Oktoba 2016

Huyu ndiye Mc Jack Abdon mrithi wa Diamond Plutnumz!

Mc Jack Abdon akiwa amepozi

Mziki wa wa bongo flavour ni mziki ambao hakika hautaisha na utendelea kukua vizazi hadi vizazi na hii ni kutokana na kusheheni vipaji vya damu changa. Msanii machachari anayekuja kwa kasi katika mziki huu ajulikanaye kama Mc Jack Abdon ni msanii unaeweza kusema anakuja kufanya makubwa katila mziki huu kutokana na mziki anaoufanya na umahiri wa kufanya staili zote za muziki. 

Mc ambaye anatamba na ngoma zake kama struggling na We mbaya ambazo zimepata kucheza katika baadhi ya vituo vya redio anaonekana kukonga nyoyo za mashabiki kiasi cha kumfananisha na Diamond ajaye. 

Endelea kuwa na mimi Bepari lako hapa hapa utapata ngoma zake zote kupitia hapa! 
Unaweza kumpata na kupata ngoma zake kupita whatsappp 0757151345

Diamond, Harmonize na DJ D-Ommy washinda tuzo za Afrimma 2016

 Diamond Platnumz, Harmonize na DJ D-Ommy, wameibuka washindi kwenye tuzo za Afrimma 2016, zilizofanyika Dallas, nchini Marekani Jumamosi hii.

Diamond ameibuka tuzo ya Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki, Harmonize Msanii bora chipukizi na D- Ommy, DJ bora wa Afrika.

“Team Tanzania Mungu ni mwema siku zote,” ameandika Harmonize baada ya ushindi huo.

Harmonize akiwa na Akothee aliyeshinda tuzo ya msanii bora wa kike Afrika Mashariki na Willy M Tuva

Diamond na D-Ommy hawakuwepo kwenye tuzo hizo.

Jumamosi, 15 Oktoba 2016

Diamond ana project mpya na Usher Raymond

 Spidi ya Diamond kulitafuta tobo la Marekani inatisha. Akiwa na collabo kibindoni na French Montana, Yo Gotti na Ne-Yo ambaye watakuwa na ziara ya pamoja Uingereza Disemba mwaka huu, muimbaji huyo wa ‘Salome’ ametoa hint ya mradi mwingine ujao na role model wake mwingine – Usher.

Ametoa hint hiyo Ijumaa hii wakati akimpongeza muimbaji huyo wa ‘No Limit’ katika siku yake ya kuzaliwa.

“Happy Birthday Bro… Can’t wait for our Big day! @usher,” ameandika kwenye Instagram.

Kwa muda mrefu Diamond amekuwa akiwataja Ne-Yo na Usher kuwa ni watu anaowaangalia sana.

Alhamisi, 13 Oktoba 2016

Diamond atoa zaidi ya Tsh milioni 40 kununua mixer kubwa ya ‘Wasafi Records’

Mkali wa wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz amesema ameagiza mixer kubwa nje ya nchi ili kuboresha studio ya ‘Wasafi Records’ ambayo tayari imeshaanza kushafanya hits kadhaa ambazo zinafanya vizuri katika chart mbalimbali za muziki nchini.

Muimbaji huyo wiki hii alitembelewa ofisini kwake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba na kumueleza mambo mbalimbali ambayo atayafanya ili kuboresha ofisi hiyo.

“Kwa sasa tunasubiri mixer ifike kwa sababu tuliambiwa hatuwezi kuichukua dukani mpaka tutoe order wakutengenezee,” Diamond alimwambia Waziri January. “Zingekuwa ni zile ndogo ndogo wangenipa lakini kwa sababu hii ni kubwa sana lazima utoe order, na tayari nimeshalipia kama dola 20,000 na kitu,”

Pia Waziri January Makamba alimsifia producer wa ‘Wasafi Record’ Lizer kwa kufanya maajabu kwenye wimbo mpya wa Diamond ‘Salome’ ambao kwa sasa unafanya vizuri.

Video queen wa Jike Shupa kuzaa na Juma Nature

Video queen wa Jike Shupa kuzaa na Juma NatureJuzi tar 13.10.2016 kupitia U Heard ya Clouds FM, mtangazaji Soudy Brown amepiga story na mrembo aliyeonekana kwenye Video ya star wa hit single ya Jike Shupa, Nuhu Mziwanda aitwaye Zena Abdallah ambaye ameeleza kuhusu mtoto wake ambaye inadaiwa alizaa na msanii Juma Nature


Mtoto wangu ni mkubwa ana miaka nane, Juma asingeweza kukataa mtoto wake jamani hawezi kukataa damu nzito kuliko maji anafanana naye sema tu ni mweupe sababu mimi ni mweupe. Na anampa matunzo sababu anaishi naye kwake tangu akiwa na miaka miwili:- Jike Shupa

PICHA 10: Forbes wameitaja list ya mastaa 14 waliokufa ambao bado wanaendelea kuingiza pesa nyingi zaidi

Mfalme wa zamani wa muziki wa Pop, Michael Jackson aliyefariki dunia miaka 7 iliyopita bado ameendelea kuingiza pesa nyingi kiasi cha dola za Marekani milioni 825 mwaka 2016, na kushika nafasi ya kwanza kama star aliyekufa na anayeingiza pesa nyingi zaidi.
Kwa mujibu Forbes, kilichomfanya MJ kuingiza mkwanja mrefu zaidi hata baada ya kifo chake ni baada ya kuamua kuuza hisa zake za sanaa kwenye kampuni ya Sony kwa dola za Marekani milioni 750.

Star huyo wa hit single ya Thriller alinunua hisa za kampuni ya muziki ya Fab Four mwaka 1984 kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 47.5 na kisha kuuza asilimia 50 ya hisa zake kwa kampuni ya Sony mwaka 1995 kwa dola milioni 115.
Mastaa waliotajwa kweny list hiyi ni hawa hapa.
1: Michael Jackson – $825 million
2: Author and cartoonist Charles Schulz – $48 million
3: Golfer Arnold Palmer – $40 million
4: Elvis Presley – $27 million
5: Prince – $25 million
6: Bob Marley -$21 million
7: Theodor ‘Dr. Seuss’ Geisel – $20 million
8: John Lennon – $12 million
9:  Physicist Albert Einstein – $11.5 million
10: Original pin-up girl Bettie Page – $11 million

Hili Dongo la Darasa ni kwa Diamond au?

Msanii Darasa ambaye amerudi kwa nguvu zote kwenye game ya hip hop ya bongo, amesema suala la wasanii wa sasa kusema wanafanya muziki wa biashara na siyo ule muziki unaoishi, wanakuwa wanakosea.
Darasa
Darasa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na EATV, na kusema msanii mzuri ni yule anayefanya muziki mzuri na kuacha ujiuze wenyewe kwenye biashara.
“Ni tatizo kubwa sana kwa msanii ambaye anasikika anasema hivyo mbele ya mashabiki au mbele ya mdau, kuna biashara siyo lazima umwambie mtu mi nafanya biashara hata kama unataka kufanya biashara, kwanza lazima ujali feelings, tunatengeneza muziki kwa ajili ya watu na naamini maisha yetu yanakuja kutegemea hivyo, wale watu watacare baada ya wewe kuwatengenezea production nzuri”, alisema Darasa.
Darasa aliendelea kusema kwa upande wake yeye anafanya muziki mzuri na ndiyo maana ameweza kukaa kwenye game kwa muda mrefu na kurudi kwa heshima kubwa.
“Mi nafanya muziki mzuri ndiyo maana sijawahi kusikika nikimwambia mtu nafanya biashara, nime'change' game yangu natengeneza muziki mzuri ambao unawafaa watu wangu, najua wao wata'care, nitaifanya sanaa yangu kuwa sehemu nzuri ya kuishi kwa mashabiki mpaka mimi mwenyewe”, alisema Darasa.
Kuhusu kufanya muziki kama biashara msanii Diamond Platnumz amesikika akiliongea sana kwa nyakati tofauti tofauti

Kabla ya kuachia kwenye redio, blogs wala Tv ngoma za WCB zinaanzia huku kwanza

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba wiki hii alitembelea ofisi za WCB na kuonyeshwa mambo mbalimbali ambayo yanafanyika katika kila kitengo.Tokeo la picha la wcb wasafi studio
Babu TALE
Moja kati ya sehemu ambayo muheshimiwa alipekekwa ni sehemu ambayo huwa mikutano kuhusu usambazaji wa kazi za wasanii wa WCB hufanyika.
Akiongea katika utambulisho huo, Babu Tale alisema wao katika usambazaji wa kazi za wasanii wao huanza kwa watu wa chini ambao wanapatikana mtaani.Tokeo la picha la babu tale
“Hii ni ofisi ya watu wa creative,” alisema Tale katika ubambulisho huo. “Wakati wa kutoa nyimbo mpya lazima tunakaa na kuwaza tunafanya nini na tutatoa kwa style gani ili tuanze kuukamata mtaa tunafanyaje kuhusu mtaa. Kwa hiyo tunapotoa nyimbo tunahakikisha kila mtu mtaani anayo halafu ndio tunaiachia redioni. Kwahiyo ikienda redioni watu wa mtaa watakuwa wanaisukuma ile ya redio,”
Pia Diamond alisema wanaitegemea mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa katika kusambaza nyimbo zake kwa uharaka zaidi.
Kwa upande wa Waziri January Makamba alimmwagia sifa Diamond pamoja na team yake kwa kufanya kazi nzuri.

Dully ataja idadi ya kolabo zake na Diamond Platunmz

Msanii wa muziki, Dully Sykes amesema mpaka sasa ana nyimbo sita ndani ambazo amemshirikisha Diamond Platnumz lakini hafikirii kuziachia.dully-sykes-ft-diamond-platnumz
dully-sykes-ft-diamond-platnumz
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Inde’ akiwa amemshirikisha ‘Harmonize’ wa WCB, amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa kwa sasa atakuwa anakwenda na mwendo wa kutoa kolabo tu.
“Sipo WCB Wasafi na wala sijasaini wasafi ila nipo nao karibu na nafanya kazi nao karibu, mpaka sasa nimefanya kazi zaidi ya sita na Diamond Platnumz na sifikirii kama zitatoka saizi,” alisema Dully Skyes
Pia muimbaji huyo ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki, amesema kwa sasa ameanza maandalizi ya kazi yake mpya ambayo pia amedai ni kolabo.

Jumatano, 12 Oktoba 2016

Baada ya Chris Brown Kenya… Sasa ni zamu ya Nicki Minaj.

 ikiwa ni baada ya mwimbaji staa wa Marekani Chris Brown kufanya show weekend iliyopita Mombasa, mpya ya leo imetoka kwa Gavana wa Mombasa Hassan Joho ambaye inaelezwa ndiye alidhamini tamasha la Mombasa Rocks Music Festival.

 Story kutoka 254 Kenya zinasema Gavana huyu inayedaiwa ana pesa za kutosha, ametangaza kuwa timu yake imeanza mazungumzo na uongozi wa rapper Nicki Minaj ili aje Mombasa kutumbuiza hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Nairobi Wire, Jamal Gaddafi aliyekua MC kwenye tamasha la Mombasa Rocks  Music Festival amesema amepewa taarifa na Joho, awambie mashabiki wajiandae kwa show nyingine kubwa ya Nicki Minaj.

Ripoti kutoka Kenya zinasema sababu kubwa hasa ya Gavana huyo kuwaleta mastaa wakubwa kutoka Marekani ni kutaka kukuza jina lake na kuitangaza zaidi Mombasa kwenye suala la utalii.

Salome imenipa umaarufu mara mbili - Rayvanny

Rayvanny, msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ameshirikishwa kwenye wimbo wa Salome na Diamond Platnumz, amesema 'kolabo' yake ya wimbo wa salome aliyoshirikishwa na Diamond Platnumz umempa umaarufu na mafanikio zaidi.

Ray amesema wimbo huo umemfungulia milango mingi ya kufanya show hadi nje ya nchi ikiwemo China na Marekani.

 Ray amesema “Wimbo huo umeniongezea show za nje nyingi na kolabo nyingi na wasanii wa nje ambazo watu watazisikia siku si nyingi lakini pia wimbo huo umeniongezea umaarufu sana katika jamii umaarufu niliokuwa nao mwanzo umekuwa mara mbili zaidi” alimalizia hivyo Ray.

Lakini pia Ray amesema wimbo huo wa salome haukuwa na lengo la kuzima wimbo wa msanii yeyote kwa kuwa kila mtu ana njia zake na mashabiki zake huku akiamini kuwa watu wanaoweza kuzima wimbo wa mtu ni watangazaji au vituo vya radio lakini pia Ray hakusita kumsifia Diamond huku akisema ni mtu mwenye roho ya kipekee sana.


Diamond Ndiye Msanii Tajiri zaidi Kwa Sasa Africa Mashariki, huu ndio mtonyo anaomiliki



Jarida la Forbes la nchini marekani limetoa wasanii matajiri zaidi duniani ,Africa na kanda mbali mbali ambapo kwa upande wa Africa mashariki.

Diamond platinum ameongoza kwa kuwa na utajiri wa dollar million 4.5 ambazo ni zaidi ya bilioni 10 za kitanzania hasa baada ya kununua Nyumba yake ya south Africa.

Vitu vingine anavyomiliki ni Majumba ya kifahari Dar,Magari ya kifahari , Berber shop, Maduka ya nguo za mitindo ya kisasa na vingine Vingi.

Amefatiwa na Dr Jose Kamilioni wa Uganda ambaye anakadiliwa kuwa na utajiri wa dollar milioni 3.9 ... Wanafatia Akothee na Jaguar anashika nafasi ya 4

Wanachokiangalia zaidi sio pesa kwenye account Bali thamani ya vitu anavyomiliki.....

Katika jarida hilo linaonyesha diamond akiwa anafanya wastani wa show 2 kwa wiki show 8 kwa mwezi na show 100 kwa mwaka ambapo show yake ya chini anakadiriwa kulipwa wastani wa dollar elfu 20,000 na show ya juu analipwa wastani wa dollar elfu 75,000 .

Mikataba yake na makampuni kama Cocacola,Vodacom na DSTV

Jarida ilo linaonyesha pia diamond anaweza vaa vitu vyenye thamani ya dollar laki 150,000 ambazo ni zaidi ya milioni 350,000,000 za tanzania mwilini mwake kwenye shoo moja ambavyo ni Pete,cheni,viatu kofia,shati na suruali na vingine.

Mahusiano ya Young Dee na Amber Lulu hadharani

Mahusiano ya Young Dee na Amber Lulu hadharani


Ukimwaga mboga wenzio wanamwaga ugali. Ukweli wafahamika baada ya mara kadhaa rapper Young Dee kukanusha kuwahi kuwa na mahusiano na video vixen kutoka kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Amber Lulu.

Akiongea na U-Heard ya Clouds FM, Amber Lulu amefunguka ukweli kwa kusema kuwa amekuwa na mahusiano na rapper huyo kwa tangu miaka minne iliyopita wakati akiwa mkoani Mbeya.

“Marafiki zangu wanajua ni jinsi gani nilivyokuwa naishi naye, mara ya mwisho alikamatwa na polisi mimi ndio nilienda kumtoa ndugu zake wote walikataa kwenda, Mimi nimeenda. Matatizo yangu yeye anayafurahia ina maana. Sikuwa nimefanya vile kwa kuwa alikuwa ni mpenzi wangu ni mtu ninayemfahamu siku nyingi na ambaye tupo wote,” amesema Amber.