Msanii wa muziki, Dully Sykes amesema mpaka sasa ana nyimbo sita ndani
ambazo amemshirikisha Diamond Platnumz lakini hafikirii kuziachia.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Inde’ akiwa
amemshirikisha ‘Harmonize’ wa WCB, amekiambia kipindi cha Planet Bongo
cha EA Radio kuwa kwa sasa atakuwa anakwenda na mwendo wa kutoa kolabo
tu.
“Sipo WCB Wasafi na wala sijasaini wasafi ila nipo nao karibu na nafanya
kazi nao karibu, mpaka sasa nimefanya kazi zaidi ya sita na Diamond
Platnumz na sifikirii kama zitatoka saizi,” alisema Dully Skyes
Pia muimbaji huyo ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki, amesema kwa sasa
ameanza maandalizi ya kazi yake mpya ambayo pia amedai ni kolabo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT