Kumbe Davido, Chidnma na Nyashinski walia kutumbuiza Fiesta! | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumanne, 14 Novemba 2017

Kumbe Davido, Chidnma na Nyashinski walia kutumbuiza Fiesta!



Fiesta ni moja kati ya tamasha ambalo limekuwa likiteka vichwa vingi vya habari kutokana na kukutanisha wasanii wengi kwa pamoja ambao wamekuwa wakizunguka katika mikoa kibao.

Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amefunguka kuwa kuna baadhi ya wasanii wakubwa Afrika wamekuwa wakiomba kutaka kutumbuiza katika jukwaa la tamasha hilo kwa mwaka huu akiwemo Davido, Chidnma, Nyashinski na wengine.
Akiongea katika kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV, Ruge amesema kwa mwaka huu ambao katika tamasha hilo hakuta kuwa na msanii yoyote kutoka nje ambaye atatumbuiza ndio ameuona ukubwa wa tamasha hilo kutoka kwa baadhi ya wasanii wakubwa ambao wamekuwa wakimpigia simu kuomba kupata nafasi ya kufanya show.
Ruge ameongeza kuwa walikuwa wakilipa kiasi kisichopungua dola laki moja kwa kila msanii mkubwa kutoka Marekani ambaye alikuwa anakuja kutumbuiza katika tamasha hilo akiwemo Rick Ross, TI na wengine.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT