Watu wengi katika miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi.

Kinachowasumbuwa wanaume na hata wanawake siyo kitambi tunasema ni
mrundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla
kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito
kumbe ni mafuta mengi.
Hivi ni visababishi vya tumbo kwa kina mama:

Vyakula feki (Junk food)
Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi
Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala
Kukaa masaa mengi kwenye kiti
Kutokujishughulisha na mazoezi
Mfadhaiko (stress)
Kula wali kila siku
Ugali wa sembe
Kula vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (chipsi, maandazi, na vinginevyo vinavyofanana na hivi.)
Hivi ndio vyakula vinavyoondoa mafuta kwenye tumbo kwa wanawake
1. ASALI NA LIMAU
Tumia asali kijiko kikubwa kimoja cha chakula na majimaji ya limau
vijiko vikubwa viwili, changanya hivi viwili ndani ya glasi moja (robo
lita) ya maji ya uvuguvugu na unywe yote mara tu ukiamka asubuhi.
2. MAJI YA UVUGUVUGU
Kunywa maji ya uvuguvugu kama lita 1 hivi wakati tumbo likiwa tupu
hasa asubuhi ukiamka tu. Hii inasaidia kusafisha mwili na kuondoa mafuta
yasiyohitajika.
3. NYANYA
Kula nyanya ambazo hazijapikwa pia inasaidia kupunguza tumbo kwa kina
mama, hivyo kula kachumbali ya kutosha kila siku ya nyanya peke yake na
utaona mabadiliko.
4. TANGAWIZI
Chemsha chai ya tangawizi, ipua na usubiri ipowe kidogo, ongeza asali
mbichi kidogo na pilipili manga kidogo ya unga. Pata kikombe kimoja cha
chai hii kila siku asubuhi mapema ukiamka tu. Asali inasaidia kuyeyusha
mafuta wakati pilipili itauongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa
chakula.
5. SIKI YA TUFAA
Siki ya tufaa (apple cider vinegar) inasaidia kupunguza njaa na
kukufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu. Kunywa kijiko kikubwa
kimoja cha siki ya tufaa mara 1 kwa siku kila siku wakati unakula
chakula cha usiku. Kazi nyingine ya hii siki ni kuweka sawa damu sukari
mwilini hivyo ni nzuri pia kwa wenye kisukari.
6. MAJANI YA BIZARI
Majani ya bizari husaidia kuondoa sumu na takataka nyingine mwilini
kitu ambacho moja kwa moja hupelekea mlundikano mdogo wa mafuta katika
tumbo. Kunywa chai ya majani ya bizari kila siku asubuhi, ukikosa majani
unaweza kutumia hata unga wake.
8. ILIKI
Iliki hufanya kazi ya kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa
chakula na ni dawa nzuri sana ya kuondoa sumu na takataka nyingine
mwilini. Iliki pia hutumika katika kupunguza uzito. Tengeneza chai yenye
iliki kila siku ndani yake, pia ni kiungo karibu kwa vyakula vingi
hivyo hakikisha unaiweka katika kila chakula unachopika kwa matokeo
mazuri zaidi.
9. MDALASINI
Mdalasini hufanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini. Chukua kijiko
kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na uweke ndani ya glasi 1 ya maji ya
moto na uache kwa dakika 5 hivi. Ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali
mbichi ndani yake na ukoroge vizuri, kisha unywe huo mchanganyiko wote
asubuhi ukiamka tu.
10. JUISI YA LIMAU
Kunywa maji ya limau au juisi ya limau kila mara kutakusaidia kuondoa
mafuta tumboni kwa haraka sana. Ongeza majimaji ya limau vijiko vikubwa
viwili ndani ya glasi 1 ya maji na uongeze punje 1 ya chumvi ya mawe,
koroga vizuri na unywe asubuhi ukiamka tu kila siku.
11. KITUNGUU SWAUMU
Ili kupunguza mafuta tumboni katakata vipande vidogo vidogo (chop) punje
3 mpaka 4 za kitunguu swaumu na unywe na maji vikombe viwili asubuhi tu
na kisha shushia na glasi moja ya maji yenye limau kidogo kwa mbali.
Hii ndiyo njia nzuri kabisa ya asili ya kuondoa mafuta tumboni kwa
haraka zaidi.
12. TIKITI MAJI
Tikiti maji lina asilimia 82 za maji kitu kinachofanya tumbo lako
kutokuwa na njaa ya kuhitaji chakula. Tikiti maji lina vitamini C ambayo
ni mhimu kwa afya bora. Kula tikiti kila siku.
13. MAHARAGE
Kula maharage kila mara kunasaidia kupunguza mafuta katika tumbo.
Maharage yana kiasi kingi cha nyuzinyuzi (faiba) kitu kinachosaidia
tumbo lako kutojisikia njaa na hivyo itakuwezesha kula chakula kiasi
kidogo. Kadri unavyokula chakula kichache ndivyo unavyokuwa mbali na
uwezekano wa kuzalisha mafuta mengi tumboni.
14. TANGO
Tango lina asilimia 96 za maji na asilimia zinazobaki ni nishati.
Tumia kachumbali yenye tango ndani yake kila siku au kula tu tango moja
kila siku ili kupunguza mafuta tumboni kwa haraka.
15. PARACHICHI
Parachichi ni tunda lingine zuri sana kwa ajili ya kuchoma mafuta
yaliyozidi mwilini. Parachichi ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (faiba).
Parachichi huikimbiza mbali njaa na wewe. Parachichi lina mafuta lakini
ni mafuta mazuri (monounsaturated fatty acids) ambayo yenyewe husaidia
kuchoma mafuta na hivyo kuondoa mafuta mabaya tumboni kirahisi zaidi.
16. TUFAA
Kula tufaa maarufu sana kama ‘apple’ (epo) kunaweza kusaidia kupigana
na magonjwa mengi sana mwilini na inaweza pia kusaidia kuondoa mafuta
kwenye tumbo lako. Tufaa hukufanya ujisikie umeshiba sana kwa masaa
mengi sababu lina potasiamu na vitamini nyingi sana ndani yake.
17. MAFUTA YA SAMAKI
Huwenda yakakulera harufu yake ila mafuta ya samaki ni mbadala mzuri
kabisa katika kuchoma mafuta ya tumboni. Mafuta ya samaki yenyewe
hulenga kuyachoma moja kwa moja mafuta yanayozidi tumboni.
18. SIAGI YA KARANGA
Siagi ya karanga hupunguza njaa na kuongeza nguvu katika mfumo wa
mmeng’enyo wa chakula. Siagi ya karanga ina kiinilishe kijulikanacho
kama ‘niacin’ ambacho chenyewe huzuia mafuta kujilundika tumboni. Hivyo
kwenye mkate wako asubuhi ningekushauri utumie hii siagi ya karanga
badala ya mafuta mengine ambayo si salama, pia unaweza kutumia hii siagi
ya karanga kama mafuta yako ya kuunga katika mboga nyingi unazopika
hata katika wali unaweza kutumia kama mafuta yako mbadala.
19. MAYAI
Mayai yana vitamini nyingi sana ndani yake (mayai ya kienyeji lakini)
na yana madini pia kama kalsiamu, zinki, chuma, omega -3 nk. Viinilishe
vyote hivyo katika mayai husaidia kuchoma mafuta yanayozidi tumboni.
Hivyo kula mayai asubuhi kila siku ili kuondoa na kupunguza mafuta
mwilini. Mayai pia ni moja ya vyakula vinavyomfanya mtu ajisikie kushiba
kwa muda mrefu bila kuhitaji kula kula tena.
20. CHAI YA KIJANI
Chai ya kijani maarufu kama ‘Green tea’ hufanya kazi ya kuondoa sumu
mwilini jambo linalosaidia pia kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini. Kunywa
chai hii ya kijani kila siku kutafanya ngozi yako kukua vivyo hivyo
kufanya tumbo lako kukaa sawa bila kuwa na mafuta mengi.
21. MTINDI
Ingawa mtindi unaweza kupelekea kuongeza uzito zaidi, hata hivyo
mtindi mtupu kabisa ule ambao haujaongezwa kingine chochote ndani yake
unaweza kukusaidia kupunguza mafuta tumboni. Matumizi yake kwa siku
yasizidi kikombe kimoja (robo lita). Pia mtindi ni moja ya vyakula
vinavyoweza kukufanya ujisikie umeshiba na hivyo kukuondolea njaa ya
kutaka kula.
22. JUISI YA KOTIMIRI
Juisi ya kotimiri (Parsley juice) huondoa sumu na takataka nyingine
zozote mwilini, pia huchoma mafuta na nishati. Kotimiri ni dawa nzuri
kwa matatizo mbalimbali ya figo pia kwa kuchoma mafuta mwilini.Tumia
kikombe kimoja cha juisi hii kila siku unapoenda kulala.
23. NDIZI
Ndizi pia zina kiasi kingi cha potasiamu na vitamini za aina
mbalimbali ndani yake. Ukipenda kula ndizi kila mara zinachofanya
mwilini mwako ni kuondoa ile hamu ya kutaka kula vyakula feki (fast
food). Zaidi sana ndizi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
na hivyo kupelekea mafuta ya tumboni kuyeyuka kirahisi zaidi. Kula ndizi
kila siku ukiweza ukiamka tu kula ndizi zilizoiva 3 mpaka 5 kila siku.
24. MAJI YA KUNYWA
Kunywa maji ya kutosha kila siku kunasaidia pia kupunguza uzito.
Kunywa maji lita 2 mpaka 3 kila siku iendayo kwa Mungu. Kunywa maji
kidogo kidogo kutwa nzima. Hili halitafanya kazi ya kusafisha mwili tu
bali pia litafanya ngozi yako kung’aa na kukuwa. Nywele zako pia
zitaonekana ni zenye afya na mwili mzima utakuwa ni wenye kuvutia.
Kitu cha kwanza ukiamka tu ni kunywa maji glasi 2 na uendelee hivyo
hivyo glasi moja moja kila baada ya lisaa limoja au mawili kutwa nzima.
Maji ni uhai, bila kunywa maji kila siku ni sawa na kwenda dukani bila
hela mfukoni.
Asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 ya ubongo wako ni maji,
asilimia 27 ya mifupa yako ni maji, asilimia 75 ya mwili wako ni maji.
Sehemu kubwa ya dunia hii imefunikwa na maji na sehemu yenye ardhi ni
kipande kidogo sana. Haijalishi unaishi kwenye baridi au kwenye joto
hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku, huhitaji kusikia kiu au
hamu ndipo unywe maji, hapana maji ni lazima uyanywe tu hata iweje.
25. MAZOEZI YA KUTEMBEA
Mazoezi ni jambo la lazima kwa mtu yeyote iwe unaumwa au huumwi.Ili
kuchoma mafuta mwilini kwa haraka zaidi tembea kwa miguu mwendo kasi
kidogo lisaa limoja kila siku. Kumbuka ni lisaa limoja yaani dakika 60
bila kupumzika (none stop) kila siku. Kutembea kwa miguu lisaa limoja
huamsha mwilini kimeng’enya kijulikanacho kama ‘lipase’ ambacho chenyewe
huamka tu ikiwa utatembea bila kusimama kwa dakika 60 na kikishaamshwa
(when it is activated) huendelea kuchoma mafuta mwilini kwa masaa 12
mfulululizo.

Chanzo Dr Fadhil Paulo.