Jinsi ya Kupambana na Magonjwa ya Nyanya | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumatano, 9 Novemba 2016

Jinsi ya Kupambana na Magonjwa ya Nyanya

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjVd7YBbV2koig_At7MOtzVUXGjkrm4Mpn7YmvT1cvOxsyttX0KB_EM7ctldHa3-LADM31dzxCXM6kymrxYL4WA6qdyBkZDNQTvxsxlhCvz2-i7ykrq0oqbOCM64JpKlm0c8w05g3f9ohk/s1600/Tomato+Bravo+F1.jpg

Furaha yangu kubwa ni pale ninapogundua kuwa msomaji wangu umeamka salama na umepata fursa hii adhimu ambayo sio wote wanaipata ya kufungua ukurasa huu nakupata maarifa mapya kila siku. Ni jambo la kumshukuru Mungu kwani wapo wengi wanaotafuta mada kama hizi ziwasaidie katika mambo yao iwe biashara, kazi au kilimo na ufugaji lakini hawazipati na wengine huzilipia pesa kwa wataalamu. Karibu tujumuike katika mada ya leo kuhusu magonjwa ya nyanya.
Utangulizi
Nyanya ni zao la chakula na biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote (masika na kiangazi), na faida hupatikana haraka na ni ya kuridhisha ikilinganishwa na mazao mengine.
Pamoja na umuhimu wa zao hili, wadudu waharibifu na magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili mkulima aweze kupata faida na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia udhibiti wa magonjwa na wadudu wa zao hili. Kipeperushi hiki kinatoa maelezo ya udhibiti wa magonjwa na wadudu muhimu ya zao la Nyanya.

MAGONJWA YA NYANYA
http://beparilakihaya.blogspot.com
Bakajani chelewa (Late blight)
Ugonjwa huu huenenzwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na hali ya hewa hasa ya unyevunyevu, na huenezwa na upepo. Majani, shina, matunda hushambuliwa. Majani huwa na ukungu mweupe na kijivu, na baadaye hukauka. Matunda huwa na mabaka ya kikahawia na baadaye kuoza. Mashina pia huwa na mabaka ya kikahawia.
Udhibiti
Nyunyiza dawa ya kuzuia ukungu hasa wakati wa masika, Dawazinazopendekezwa ni Ridomil, Dithane 45, Bravo, Funguran, milraz.Fanya mzunguko wa mazao. Usipande nyanya sehemu moja kila msimu aupalipolimwa mazao jamii ya nyanya km viazi mviringo, bilinganya, aina zoteza pilipili na nyanya chungu.Tumia mbegu safiPanda aina za nyanya zinazovumilia ugomjwa
http://beparilakihaya.blogspot.com
Bakajani tangulia (Early blight)
Huenezwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na kuenezwa na hali ya hewa pamoja na mbegu zenye ugonjwa. Mabaka ya kahawia yenye mistari ya mviringo huonekana kwenye majani na shina. Baka jeusi hutokea sehemu ya tunda inayoshikana na kikonyo.
Udhibiti
Nyunyiza dawa ya Kocide, FunguranTeketeza mabaka ya mazao baada ya kuvunaTumia mbegu safi na bora
http://beparilakihaya.blogspot.com.
Mnyauko fusari (Fusarium wilt)
Huenezwa na mbegu zenye ugonjwa. Husambazwa na vimelea vya fungasi vinavyoishi kwenye udongo.
Ugonjwa hujitokeza zaidi wakati wa kiangazi. Vimelea hushambulia sehemu au
mirija ya mmea ya kupitishia maji na chakula. Mmea hukosa maji na chakula na
hatimaye hunyauka. Shina la mmea likipasuliwa ndani huonekana rangi ya kikahawia.
Udhibiti
Tumia mbegu safi na boraTumia mzunguko wa mazao. Nyanya zisizungushwe na mazao jamii yakeTeketeza masalia ya mimeaChoma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu
http://beparilakihaya.blogspot.com
Mnyauko bacteria (Bacterial wilt)
Ugonjwa husababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye udongo. Huenezwa na kusambazwa na mbegu na udongo wenye vimelea. Mirija ya mimea ya kupitishia maji na chakula hushambulia na mimea hunyauka ghafla. Mmea hukauka na kufa.
Udhibiti
Panda mbegu safiPanda nyanya sehemu ambayo haijawahi kupandwa viazi mviringo,bilinganya au nyanya chunguTumia mzunguko wa mazaoHakikisha mfereji wa maji ya kumwagilia hayapiti kwenye shamba lenyehistoria ya ugonjwa huu.Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu
http://beparilakihaya.blogspot.com
Mnyauko vetisili (Verticillum wilt)
Hakuna dawa inayozuia au kutibu ugonjwa huu kwa sasa. Ugonjwa husababishwa na ukungu (fangasi) kwenye udongo. Ukungu huu huishi kwenye udongo kwa muda mrefu bila kudhurika. Ugonjwa huongezeka ikiwa mizimizi ya nyanya imeshambuliwa na minyo fundo; au kukiwepo na hali ya ubaridi au ukame. Ugonjwa husababisha hasara kubwa. Ugonjwa hushambulia sehemu ya ndani ya shina na kusababisha sehemu hiyo kuwa na rangi ya kijivu. Majani hugeuka njano na mimea
kunyauka na kufa.
Udhibiti
Tumia mzunguko wa mazao usiopungua miaka mineOndoa mabaki ya nyanya shambaniTumia mbegu bora na safi
http://beparilakihaya.blogspot.com
Bakadoa (Bacterial spot)
Ugonjwa huu huenezwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu, pia kwenye hewa. Huenezwa kwa kasi sana wakati wa masika. Madoa ya rangi kahawia huonekana kwenye majani na matunda.
Udhibiti
Panda mbegu bora na safiTumia mzunguko wa mazaoTeketeza masalia ya mazaoNyunyizia dawa ya funguran, Kocide101, Cobox, Bravo
http://beparilakihaya.blogspot.com
Makovu bakteria (Bacterial canker)
Ugonjwa huenezwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu na hewani. Hutokea zaidi wakati wa masika. Majani hukauka nchani na makovu yaliyodidimia hutokea kwenye shina. Matunda huwa na makovu yenye rangi ya kahawia sehemu ya katikati.
http://beparilakihaya.blogspot.com
Udhibiti
Tumia mbegu bora na safiwww.ariuyole.go.tz 2Teketeza masalia ya mazaoTumia mzunguko wa mazaoRasta (Yellow leaf curl)
Ugonjwa huu husababishwa na virusi na huenezwa na nzi wadogo weupe. Hutokea zaidi wakati wa kiangazi. Mimea hudumaa na majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya manjano na pengine rangi ya zambarau. Nyanya hupasuka.
Udhibiti
Nyunyiza dawa za sumu za kuua wadudu (Selecron, Dursburn, Actelic)Ng’oa mimea yenye ugonjwaTumia mzunguko wa mazaoWeka shamba katika hali ya usafi
http://beparilakihaya.blogspot.com
Batobato (Tomato mosaic virus)
Ugonjwa husababishwa na virusi na hueezwa na mbegu na kugusana. Majani huwa na mchanganyiko wa rangi hasa kijani kibichi na kijani kilichofifia (majano). Majani hujikunja na manjani machanga huwa na maumbile yasiyo kawaida. Ukifikisha jani huwa linavinjikavunjika.
Udhibiti
Tumia mbegu bora na safiNg’oa mimea iliyoshambuliwaTeketeza masalia ya mazaoWeka shamba katika hali ya usafi
WADUDU WAHARIBIFU
http://beparilakihaya.blogspot.com
Viwavi Matunda (Fruit worm)
Viwavi hawa hutokana na wadudu nondo. Viwavi hutoboa matunda na kuacha matundu na hatimaye matunda huoza. Hupunguza ubora wa matunda.
Udhibiti
Nyunyizia dawa ya kuua wadudu. Dawa hizo ni pamoja na Actelic 50EC, Selectron,
Dursbaan, Maji ya majani ya mwarobaini au utupa pia huua wadudu.
http://beparilakihaya.blogspot.com
Utitiri wekundu (Red Spider mites)
Hawa ni wadudu wekundu, wadogo sana wanaoweka utando chini ya majani, hasa wakati wa kiangazi. Wadudu hawa hufyonza utomvu kwenye majani na kusababisha majani kukauka.
Udhibiti
Nyunyizia dawa za sumu. Dawa hizo ni pamoja na Actellic, Selecron,Dursbarn na ThionexMwagilia maji mara kwa maraWeka shamba katika hali ya usafi
http://beparilakihaya.blogspot.com
Inzi weupe (White flies)
Hawa ni Inzi weupe wadogo sana. Hujitokeza sana wakati wa kiangazi. Hueneza ugonjwa wa virusi ujulikanao kama Rasta.
Udhibiti
Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Selecron, Actellic, Dursban na
thionex. Pia maji ya majani ya mwarobaini na utupa.
http://beparilakihaya.blogspot.com
Vidukari au Wadudu mafuta (Aphids)
Ni wadudu wenye rangi nyeusi au kuijani au kahawia. Hukaa chini ya majani na kufyonza utomvu kwenye majani machanga. Hudumaza mmea na kushindwa kuzaa matunda
Udhibiti
Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Rogor, Actellic, Selecron, Dursban
maji ya majani ya mwarobaini na utupa, maji ya pilipili.
http://beparilakihaya.blogspot.com
Minyoo (Nematodes)
Ni minyoo midogomidogo ambayo hushambulia mizizi na kuweka vifundo. Mizizi hushindwa kuchukua maji na chakula kwenye udongo. Mimea hudumaa na kushindwa kuzaa
Udhibiti
Tumia mzunguko wa mazaoChoma udongo wa kitalu kabla ya kusia mbegu kwa kutumia karatasi laplastiki jeusi na nishati ya juaChoma masalia ya mazao
http://beparilakihaya.blogspot.com
Sota (Cutworms)
Hushambulia miche ya nyanya hasa baada ya kupandikizwa shambani. Wakati wa mchana hujificha kwenye udongo na usiku hujitokeza na kukata miche kwenye shina usawa wa udongo.
Udhibiti
Nyunyiza dawa za kuua wadudu kwenye shina usawa wa udongoHakikisha miche inapata maji ya kutosha.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT