Bila shaka umejaaliwa afya tele kwa siku ya leo mpenda biashara na tajiri mtarajiwa. Shukrani zake Mwenyezi Mungu kwa kutujalia hilo. Katika muendelezo wa kupeana mbinu mbali mbali za kufanikiwa katika biashara leo hii nakupa Swali Moja Muhimu La Kujiuliza Kwenye Biashara Yako Kila Siku Ili Ufanikiwe. Karibu tuwe pamoja tuvune kitu hapa.
Kuna vitu viwili ambavyo vimekuwa vinawachanganya wafanyabiashara walio wengi. Vitu hivyo ni LENGO na DHUMUNI. Lipi lengo la biashara na lipi dhumuni la biashara. Hivi ni vitu viwili ambavyo vinakaribiana lakini havipo sawa. Tutaviangalia hapa vizuri ili tuweze kuchukua hatua sahihi.
Kuna vitu viwili ambavyo vimekuwa vinawachanganya wafanyabiashara walio wengi. Vitu hivyo ni LENGO na DHUMUNI. Lipi lengo la biashara na lipi dhumuni la biashara. Hivi ni vitu viwili ambavyo vinakaribiana lakini havipo sawa. Tutaviangalia hapa vizuri ili tuweze kuchukua hatua sahihi.
DHUMUNI la biashara ni ule msukumo uliopo ndani ya mfanyabiashara, kitu ambacho anataka kukitoa kwa wengine ambacho kitayafanya maisha yao kuwa bora zaidi. Dhumuni la biashara ndiyo linawafanya watu waendelee kukomaa na biashara hata pale ambapo wanakutana na changamoto.
LENGO la biashara linategemea na mfanyabiashara mwenyewe. Malengo ya biashara yanaweza kuwa mengi, kutengeneza faida, kuonekana kwamba upo, kujenga umaarufu, kuwa tajiri, kujitengenezea ajira na kadhalika.
Hivyo kwa biashara yoyote unayoifanya, vijue vitu hivi viwili kwa uwazi, DHUMUNI la wewe kuwa kwenye biashara hiyo na MALENGO yako kwenye biashara hiyo. Hivi ni vitu viwili vinavyojenga msingi wa biashara yako. dhumuni litakupa nguvu na msukumo wa kuendelea hata pale unapokutana na changamoto. Malengo yatakupa hamasa ya kuweka juhudi ili kuweza kuyafikia. Vitu hivi viwili ni muhimu.
Leo tunakwenda kuangalia swali moja muhimu ambalo kila mfanyabiashara anapaswa kujiuliza kila siku kwenye biashara yake ili aweze kufanikiwa. Swali hilo linaleta pamoja DHUMUNI na LENGO la biashara yako.
SOMA: Njia Tano(5) Za Kukuwezesha Kuziona Fursa Nyingi Zaidi Za Kibiashara.
SOMA: Njia Tano(5) Za Kukuwezesha Kuziona Fursa Nyingi Zaidi Za Kibiashara.
Swali unalopaswa kujiuliza kila siku kwenye biashara yako ni hili; NINAONGEZAJE THAMANI KWA WATEJA WANGU?
Hili ni swali muhimu sana kwa ukuaji wa biashara yako, kwa sababu bila ya wateja hakuna biashara, na kama hutoi thamani huwezi kupata wateja wa biashara yako.
Kumbuka ya kwamba wateja hawanunui kwa sababu wewe unauza, bali wananunua kwa sababu wana shida au wana mahitaji ambayo wanafikiria wewe unaweza kuyatatua. Hivyo ukiweza kuyatatua matatizo yao na kutimiza mahitaji yao wataendelea kuwa wateja wazuri kwako. Lakini ukishindwa kutatua matatizo yao watakwenda sehemu nyingine ambapo watapata kile wanachotaka.
Hii ndiyo sababu kubwa ya kukufanya wewe ufikirie kuongeza thamani kwa wateja wako mara zote. Usimwangalie mteja kama mtu anayeleta fedha kwenye biashara yako, bali mwangalie kama mtu ambaye wewe umejitoa kumpatia huduma bora za kutimiza mahitaji yake. Mara zote ongeza thamani kwa mteja wako, yafanye maisha ya mteja wako kuwa bora zaidi kupitia biashara ambayo unaifanya wewe.
Hata kama unafanya biashara ya uchuuzi, ambapo unauza kile ambacho kila mtu anauza, bado unaweza kuongeza thamani kubwa kwa wateja wako kwa jinsi unavyowahudumia, namna unavyoongea nao, unavyojibu maswali yao, unavyotabasamu na hata unavyowakaribisha tena kwenye biashara yako.
Nina uhakika umewahi kwenda kwenye biashara fulani na ukatika hapo ukiwa unajisikia vibaya na hovyo kwa namna ambavyo hukujaliwa na watoaji huduma wa biashara ile. Na pia umewahi kwenda kwenye biashara fulani na ukatoka ukiwa na furaha na hamasa ya hali ya juu. Tofauti hizi zinatokana na thamani ambazo wafanyabiashara wameweka kwenye biashara zao.
SOMA: Njia za Kupata Faida Katika Biashara Bila Kukwepa Kodi
Kila wakati angalia namna unavyoweza kuongeza thamani kwa wateja wa biashara yako. Hakuna mtu ambaye hapendi thamani na hivyo utawaalika watu wengi zaidi kuwa wateja wako kama utakuwa tayari kutoa thamani kubwa.
SOMA: Njia za Kupata Faida Katika Biashara Bila Kukwepa Kodi
Kila wakati angalia namna unavyoweza kuongeza thamani kwa wateja wa biashara yako. Hakuna mtu ambaye hapendi thamani na hivyo utawaalika watu wengi zaidi kuwa wateja wako kama utakuwa tayari kutoa thamani kubwa.
Jua dhumuni kuu la biashara yako na pia yajue malengo yako, kisha angalia namna unavyoongeza thamani kwa wateja wako ili uweze kufikia malengo na madhumuni yako ya kibiashara. Usikubali mteja aondoke kwenye biashara yako akiwa amejisikia vibaya na hovyo, utakuwa umekubali kumpoteza mteja huyo na wengine wa karibu yake.
Mara zote ongeza thamani kwa wateja wa biashara yako, ni njia rahisi na ya uhakika ya kukuza biashara yako.
PENDA BIASHARA, JIFUNZE BIASHARA.
Karibu tena hapa kila siku kwa mada mpya za kukujenga kimafanikio na usisahau kushea na wenzako ukurasa huu nao wafaidike. Tutoke pamoja.
Karibu tena hapa kila siku kwa mada mpya za kukujenga kimafanikio na usisahau kushea na wenzako ukurasa huu nao wafaidike. Tutoke pamoja.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT