Hatua Saba za Kukuwezesha Kufikia Malengo Yako. | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumamosi, 17 Desemba 2016

Hatua Saba za Kukuwezesha Kufikia Malengo Yako.

Ni  jambo la muhimu sana kuwa na malengo  ya maisha yako. Changamoto kubwa kwa wengi  ni namna gani watayafikia malengo hayo ambayo wamejiwekea. Wengi wamekuwa na malengo makubwa ambao yamebaki kuzunguka kwenye mawazo na kwenye akili zao tu. Wameshindwa kabisa kuyafanya kuwa halisi. Kwanini na wewe uendelea kushuhudia haya yakiendelea kukukumba na wewe? Inuka tafadhali badili mtizamo wako na ufikie malengo yako. Usipoinuka na kuangalia mambo na kufanya kwa utofauti bila shaka na wewe utakuwa kama wengi wanavyobaki  na malengo bila kutimia. 
Leo hii kama kila mtu angejaribu kuyafanyia kazi malengo yake kuwa halisi ni wazi Tanzania, na Dunia ingebadilika sana na ingekuwa sehemu bora zaidi ya kuishi.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEis-1wBzg7aX40uebAQhbuDHvUjHi46041BOCzXvvIcCy9y_EkpaBoNKeS6osXKW5tR3yTqwuGOLfg8xMdUvUp9rf-F3c63KmfFObNDWRCJpRXosKEtbZUw7s-d9qfX4oaThKSGQjtsYePa/s1600/dat.jpg
Kimisingi  umeshindwa kufikia malengo si kwa sababui nyingine yeyote, la hasha! Sababu kubwa ni kwamba huna maarifa ya kutosha juu ya kufikia malengo. Au ni yawezekana hujui hatua muhimu zitakazo kufikisha kwenye malengo yako. Basi habari njema ni kwamba, umefanya uamuzi wa msingi sana kutembelea mtandao huu na kusoma makala hii. Nina imani kuanzia sasa utaondoa ukungu mbele yako. Maana nitakujuza hatua muhimu za kufanyia kazi uli uone malengo yako yakitokea. Hatua hizi zinatoa hakikisho la wewe kufikia lengo lolote maishani mwako,  kama ni lengo la kukuza kipato, au lengo kuwa bora kiroho, au lengo la kuwa mtu maarufu, chochole ambacho ni lengo kwako ni lazima ufike kwa kutumia hatua hizi. 
            
 Zifuatazo ni hatua muhimu zitakazokuwezesha kufikia kilele cha malengo yako. Tafadhali tuendelee.........................
   1. Amua Nini Unataka.
Kuamua unachotaka ni hatua ya awali inayokupa fursa ya kunyambua unachokitaka kwenye maisha yako kutoka kwenye kapu kubwa la mawazo na fikra. Fanya uamuzi na ujiridhishe kwamba uchaguzi utakaoufanya ni mahitaji yako kutoka ndani mwako, na mara zote iwe ni kitu unachokipenda kabisa na unajisikia amani na furaha nyuma yake. Kama huna uakika ni vyema ukaendelea kujifunza zaidi juu ya mambo ya msingi kuhusu kitu hicho ili upate fursa ya kufanya uamuzi ukiwa na taarifa zote.
    2. Andika Malengo Yako.
Iko nguvu kubwa kati ya ubongo na mkono wako unapoandika malengo yako. Kwa kuandika malengo yako unatoa fursa ya akili kushughulika juu ya malengo uliyoyaandika. Tendo hili la kuandika linaruhusu nguvu ya kanuni  ya matarajio, kanuni ya mvuto,  na kanuni ya mawasiliano kwa pamoja kuanza kazi kati ya akili na ulichokiandika. Pia inakupa imani, na uhakika wa kwamba utafikia malengo yako.
    3. Kuwa Tayari Kulipa Gharama.
Ni vyema kujua kwamba hupati kitu bila ya kulipa gharama. Yaani kwa kifupi ni kwamba hakuna kitu cha bure. Vitu vyote ukivihitaji lazima ulipe gharama tena sio gharama tu bali gharama stahiki. Ukilipa gharama kidogo uwe na uhakika utapata kinachoendana na malipo yako. Sasa ufanyeje hapa, sikia! andika orodha ya gharama utazopaswa kuzilipa ili kufikia malengo yako. Andika kwa umakini ili ziwe ni gharama halisi zitakazokufikisha kwenye malengo yako. Kumbuka gharama hizi sio lazima ziwe za kifedha la hasha! Inaweza kuwa mazoezi, muda, juhudi kazini, kujali muda, kusoma zaidi, kusali sana, kufunga na kadhalika.
Mfano,  unawezakuta gharama za kufikia malengo yako ni kuamka mapema sana kila siku na kujihamasisha,  au kufanya kazi kwa bidii zaidi;  au ni  kuongeza ujuzi au maarifa au elimu ulionayo. Wewe andika yote. Au unatakiwa kubadili biashara au kazi au tasnia uliyoko ndiyo ufanikiwe. Wewe andika tu. Yote hayo unayaandika chini ya lengo lako ulilolichagua. Kumbuka tunachokifanya hapa ni kuifanyasheria ya kupanda na kuvuna ishughulike, maana lazima ghrama zilipwe. Yaani lazima upande mbegu aridhini, uzimwagilie ndipo uvune. Au ni lazima utoe ndipo upokee.
4. Tengeneza Mpango Kazi. 
Tengeneza mpango kazi kwenye maandishi. Kumbuka uwezo wa kuandika malengo na kuyapanga ili yatokee ndiyo mbinu kuu ya kukufanikisha.  Mpango unaanza na wewe kuorodhesha vitu vyote ambavyo unafikiri ukivifanya vitakusaidia kufikia lengo kuu. Baada ya hapo unaanza kuipanga orodha hiyo  uliyoiandika kwa kufuata umuhimu na unyeti wa kila jambo. Yaani ni kitu kipi cha muhimu kukifanya kabla ya kingine ili ufikie kwenye lengo lako? Au ni kitu gani katika orodha yako ambacho hakiwezi kufanywa kabla ya kukamilisha kingine? Basi vipange kulingana na umuhimu.
 Kufanya hivyo kutakusaidia kujua njia utayopita kufikia malengo yako. Hatua hii itakuwa inakufanya kutokuwa kwenye ulimwengu wa kubahatisha mambo kwa maana utakuwa na uhakika wa kufika tu. Hii itakuongezea uwezo na imani ya kufikia na kukuongezea mzuka na uchu wa kutamani kufikia malengo yako.
           5. Anza Kutendea Kazi Mpango Wako.
Hujaandika mpango ili ukufurahishe au kama pambo, anza kuutekeleza. Najua hapa ndipo kwenye utofauti mkubwa kati ya waliofanikiwa na wasio na mafanikio. Baada ya kutengeneza mpango wako ulioandikwa ukionesha na gharama unazoenda kulipa unatakiwa kuchukua hatua maramoja yaani kuutekeleza. Kumbuka Bibliainasema “imani bila matendo imekufa” . Matendo yatachochea kila aina ya nguvu  duniani kukufikisha unakotaka.
Unapoanza kutenda unaiwezeshakanuni ya mvuto kukusaidia kufikia unakotaka. Hii kanuni ya mvuto ndio inaowasaidia wote wanaopambana juu ya jambo fulani bila kuchoka na hatimaye wanalipata. Jaribu kuuliza wanamuziki wakubwa kwamba nini kimewafikisha walipo leo. Ndio utagundua kazi na uwezo wa kanuni hii. Kadhalika matendo yako yataionyesha dunia inayokuzunguka kwamba unamaanisha kwa kile unachokilenga.
Changamoto kubwa kwa watu wengi wakianza kutendea kazi mipango yao hufika mahali wanaanza kupunguza matendo juu ya malengo yao bila kujua kufanya hivyo kutaathiri matokeo.Tafadhali hakikisha unatenda matendo ya kutosha ili ufike bila tatizo kwenye malengo yako. Ukifanya kwa wastani kama wengi wafanyavyo utapata matokeo lakini hayatakuwa yale uliokusudia, yatakuwa yakawaida sana. Utajikuta unakamata nafasi ya pili au tatu wakati ulikusudia kushinda nafasi ya kwanza. Yaah! namba tatu inaweza ikawa ya ushindi na ukazawadiwa lakini je hilo ndilo lengo lako?
              6. Fanya Chochote Kila Siku.
Fanya chochote kila siku hasa kile kinachokupeleka kuelekea kwenye lengo lako la msingi. Hili ni kanuni muhimu ya mafanikio itakayo kujengea nguvu na shauku kubwa. Ili uendelee kuwa na moyo, ujasiri, kujiamini na mwenye hamasiko unapaswa kufanya kitu kila siku ambapo utakuwa unajihisi na kujiona unasonga mbele na kuendelea.
Kazi yako ni kuhakikisha unajijenga tabia ya kufanya jambo lolote kila siku hasa jambo linalokusogeza kufikia malengo yako. Unajua ukijitaidi kila siku kufanya kwa asilimia moja utajikuta mwisho wa mwenzi umefanya kwa asilimia thelathini au thelathini na moja. Na utakuwa umepiga hatua kubwa sana. Usikubali siku ikupite hujafanya chochote kinachokusogeza mbele kufikia malengo yako.
      7.   Komaa Usiache.
Amua  kukomaa mpaka ufikie mafanikio au malengo uliyojiwekea na kamwe kutoacha, maana umeshaanza kuelekea ndoto zako au malengo yako. Haijalishi utakutana na ugumu au vikwazo kiasi gani jihaidi kutokuacha au kutokukatisha ulichokianza. Amua hivyo tafadhali. Endelea hadi ufikie kilele. Komaa sana.
Nimefika tamati lakini sasa uko huru kufikia  malengo yoyote utakayo jiweke.  Kama utafuata hatua hizi kwa umakini, na kwa dhati huna sababu ya kuwa na wasiwasi wa kufikia kilele cha malengo yako. Nakutakia kila la  kheri katika safari yako ya mafanikio.

SOMA: Kipimo Cha Mafanikio Kabla Ya Kuanza Mwaka Mpya

 Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mali, maarifa na afya. Kazi kwako!
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT