Zikiwa zimebaki siku kadhaa ili kumaliza mwaka huu, hatuna budi
kuendelea kumuomba na kumshukuru mwenyezi Mungu azidi kutupa neema na
baraka zake ili tuumalize mwaka kwa vizuri na kuanza mwaka mpya tukiwa
ni watu wenye furaha mioyoni mwetu huku tukipanga mipango thabiti ili
tuweze kuuanza mwaka mpya vyema.
Lakini kama hiyo haitoshi maisha ya mafanikio huenda sambamba na kufanya tathimini, hatuwezi kuanza mwaka mpya, bila kufanya tathmini kwa yale ambayo tumeyatekeleza kipindi cha nyuma. Endapo utashindwa kufanya tathimini utashindwa kuelewa ni wapi ambapo ulishindwa kutimiza lengo lako.
Kufanya tathimini ni muhimu sana ili kuifanya akili yako itambue ya kwamba ni muhimu kuweka uchumbuzi yakinifu kwa mambo ambayo umeyafanya katika kipindi hiki kabla ya kumaliza siku 365 na kuanza mwaka mpya.
Inawezekana bado upo kwenye mataa na bado unashangaa uelekee wapi, wala usipate tabu kwa kuwa nataka tuweke mambo bayana ambayo yatukusaidia kufanya tathimini katika mwaka huu ambao zimesaria siku kadhaa kuisha.
Ipo hivi mwanadamu katika kila kitu lazima ajue mambo aliyoyofanya hupimwa katika njia kuu mbili ambazo ndiyo kipimo tosha cha mafanikio yako.
1. Ulichokisababisha.
Jambo la kwanza ambalo litakusaidia wewe kufanya tathimini ni kuangalia ni mambo gani ambayo uliyapanga na umekwisha yatekeleza? Si kuyatekeleza tu bali kuyatekeleza kwa ufasaha bila kujali changamoto ambazo umezipitia.
Ulichokisababisha ni mkusanyiko wa mambo yote chanya ambayo umeyafanya katika kipindi chote cha mwaka huu, hata hivyo kitu hicho ambacho umekifanya ni lazima kiwe kitu ambacho ni cha kuacha alama kwa watu wengine.

Au kama kitakuwa si cha kuacha alama, kitu hicho kitakuwa ni kitu
ambacho kitakuwa fundisho kwa wengine ambao wanakutazama wewe. Kama
umepanda miti hongera sana, kama umeanzisha biashara hongera pia, kama
umejenga nyumba hongera kama umenunua gari hongera kwako, najua fika kwa
hayo ambayo umeyafanya utasababisha utengeneze kitu kinachoitwa "wivu
wa maendeleo" najua fika alama hiyo wengi wao watajifunza kutoka kwako.
2.Ulichokisuluhisha.
Jambo la pili na la mwisho ambalo nilitaka kuzungumza nawe, ni kwamba
tathimini ya kile ulichokifanya lazima upime katika kuyatazama mambo
ambayo umeyatatua, eidha katika jamii ambayo unaishi au mambo yako
binafsi. Nazungumza katika hili nikiwa na maana siri kubwa ya mafanikio
yako ipo katika usuluhisho wa changamoto.
Kama ulianzisha jambo lolote ujue fika hilo jambo ni majibu ya
changamoto fulani, hivyo kwa namna moja ama nyingine kama endapo
ulifanya hivyo na hujaweza kufikia lengo lako, unachotakiwa kufanya ni
kuangalia sababu za msingi zilizokufanya ushindwe kufikia lengo na si
kukata tamaa.
Kwani kama utakuwa ni mwenyeji wa kukataa tamaa tambua fika mtu aitwaye
mafanikio utakuwa ni mgeni kwako. Ili kutengeneza ukaribu wa mafanikio
yako kwa mwaka ambao unataraji kuanza hivi karibuni unatakiwa kupanga
malengo yako upya huku ukibuni mbinu mpya za kuzitumia ili kufikia
malengo mapya. Kwani huwezi kufanikiwa daima kama utaendelea kutumia
njia ile ile kama unataka matokeo tofauti.
SOMA: Bila Tabia hii Sahau Kufanikiwa
Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mali, maarifa na afya. Kazi kwako!
SOMA: Bila Tabia hii Sahau Kufanikiwa
Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mali, maarifa na afya. Kazi kwako!
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT