HII NI SIRI YA MAFANIKIO YANGU....SOMA UJIFUNZE KITU NA UFANIKIWE HARAKA | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumanne, 8 Novemba 2016

HII NI SIRI YA MAFANIKIO YANGU....SOMA UJIFUNZE KITU NA UFANIKIWE HARAKA

Image result for mafanikio
Karibu tena ndugu yangu mwanamafanikio mwenzangu. Sijawa na mafanikio makubwa saaana kiasi cha kutisha ila haya niliyo nayo ni makubwa sana kwa mtazamo wangu pengine hata kwa mtazamo wa wengine ambao hawajafikia hapa. Sio kawaida yangu kuwa mchoyo na ndo maana leo nimeamua nikupe bila kinyongo siri ya mafanikio yangu. Nina uhakika siri hii inaenda kubadilisha kitu katika maisha na mafanikio yako kwa kiasi kikubwa!

Kwa muda mrefu watu wamekuwa wakiniuliza kwa nini nimefanikiwa, kwa nini nimetoka katika hatua fulani na kuingia katika hatua fulani. Nimekuwa nikiwajibu kwamba kujituma kwangu ndiyo kumenifanya kuwa hapa, kutokulala kwangu kwa muda mrefu huku nikifikiria ni kitu gani natakiwa kufanya ili nitoke kutoka hapa nilipo.

Katika kuwaambia hayo lakini pia huwa siwafichi kuhusu siri moja muhimu ambayo ilinifanya nitoke kule kwa haraka na kuja huku. Kitu hiki ndicho nitakachokwambia leo, nitataka ufanikiwe, sitaki ubaki hapo ulipo, mbegu nitakayoipanda moyoni mwako leo, nitataka ikue moyoni mwako na kuota mizizi.
Kuna kipindi sikuwa nikipenda mitandao ya kijamii kwa sababu nilijiona kuwa bize sana. Baada ya kipindi fulani, nikapata wazo la kuwaambia vijana kuhusu maisha yangu, wale waliokata tamaa, basi niwatie nguvu na kuendelea mbele.

Najua si wote wanaosoma magazeti, si kila siku nitapata nafasi kwenye gazeti. Wakati mwingine nakuwa na kitu, nikiwaambia wafanyakazi wangu ambao ni kama ndugu zangu, wananiambia kwamba nafasi imekuwa ngumu kupatikana gazetini, hivyo natulia na kufikiria siku nyingine.
Wazo la kujiunga na mitandao ya kijamii likanijia. Kama yule Michael aliyekuwa kule kusipofika magazeti, lakini si ana simu? Si anatumia Facebook? Kwa nini nisizungumze naye? Labda Esta ni mgonjwa, hawezi kutoka ndani na kwenda kununua gazeti, lakini si ana simu? Si anatumia Facebook? Kwa nini nisizungumze nao na kupitia hukohuko Facebook? Kweli nikafungua hii page.
Ndugu yangu! Nimefungua page hii kwa ajili yako, sikufungua kwa ajili ya Obama, sikufungua kwa ajili ya Bill Gates, nimefungua kwa ajili yako, Mtanzania ambaye unatamani kutoka hapo ulipo, nimefungua page hii kwa sababu nina mambo mengi ya kuzungumza pamoja nawe, kukushauri ni kipi unachotakiwa kufanya.
Rafiki yangu! Hakuna siri kubwa katika utajiri kama UTOAJI. Wazazi wangu walinifundisha kuhusu kutoa, waliniambia kwamba hata kama sitokuwa na kiasi kikubwa cha fedha, ni lazima nitoe kwa wale ambao hawana kitu.
SOMA: 
Hilo limekuwa somo bora katika maisha yangu. Nimekuwa nikifanya hivyo mara kwa mara, nimefundishwa kutoa na hivyo huwa ninawafundisha watu kuhusu utoaji.
Mungu anapotaka kumsaidia mama Halima ambaye ni masikini wa kutupwa, hamuangushii fuko la pesa mwanamke huyo mjane, anachokifanya ni kumsaidia mama Halima kupitia wewe. Mungu anampa mama Halima kupitia wewe hapo, je, utakapopewa fedha za mama Halima, utazila au utakwenda kumpa?
Wengine wanahisi kwamba kutoa ni lazima uwe tajiri, wengine wanajiona hawawezi kutoa, wanamuona Mengi, Bakhresa ndiyo watu wanaotakiwa kutoa na si wao. Ndugu yangu, hakuna baraka nyingi kama kwenye utoaji. Ni bora kutoa kuliko kupokea.
Unapotoa, Mungu hakuachi hivihivi, atakubariki maradufu. Wakati mwingine unaanzisha biashara, haziendi, kila unapoanzisha, zinafeli, umekuwa ukijiuliza tatizo ni nini, unahisi umerogwa kisa tu kuna siku ulikuta unyoya wa kuku mlangoni kwako, unahisi kuna mtu hataki ufanikiwe, kumbe ukifuatilia ni kwa sababu wewe si mtoaji.
http://beparilakihaya.blogspot.com
Mungu ametamani kuwasaidia watu wengi kupitia wewe, anakupa lakini hupeleki kunapotakiwa kwenda, mwisho wa siku, unatumia fedha zote na hapo bado unataka Mungu akufanikishe katika biashara zako.
Ndugu yangu, Mungu hafanyi kazi kwa staili hiyo. Mungu anataka akupe wewe, na wewe utoe kwa watu wengine. Kuna somo pana kuhusu utoaji na limekuwa likiwasaidia watu wengi.
Waangalie matajiri wengi, nampongeza Reginald Mengi, amekuwa mtu wa kujitoa, anasaidia wengi, kila mwaka huwa anawaita walemavu na kula nao. Ni jambo jema na huwa Mungu analiangalia sana jambo lake, na hata baraka anazozipata ni kwamba huwa anatoa.
Nimekuwa kwenye msingi wa kutoa, najua fedha anazonipa Mungu si zangu zote, nyingine huwa ni za mama Petro ambaye amekuwa akipigwa na umasikini mkubwa, nyingine huwa ni za yule mjane anayesoma na kushindwa kulipia ada.

Mungu yupo tayari kukufanya kuwa bilionea, lakini kabla hajakupa bilioni tano, je, alipokupa elfu kumi ulifanya jambo gani kwa ajili ya wengine? Anza kulifanyia kazi jambo hili kwa kutoa kwa wahitaji bila kuanza kujadili kwa nini wakose hata kama wana mikono na miguu we toa tu anayekulipa sio wao bali Mungu, na pia kuwapa bure ujumbe huu wenzio kwa kushea nao ukurasa huu na uendelee utaonamatokeo yake! Uwe na siku njema na karibu tena.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

Maoni 3 :

  1. Nimekuwa nikitaka kuwa wa ndugu mkubwa wa ILLUMINATI kama nilikuwa na hamu kubwa ya utajiri na umaarufu na kwa jitihada zangu nimeingia katika baadhi ya mikono isiyofaa kunidai kunisaidia kupata punguzo la uanachama na nimepata maradhi ya fedha yangu. Hivi karibuni nimepata ajira ya haki na wajumbe kwenye illuminatiworldofriches6666 @ gmail. com au +2349034745112

    JibuFuta
    Majibu

    1. WELCOME TO THE GREAT BROTHERHOOD.
      Do you want to be a member of Illuminati as a brotherhood
      that will make you rich and famous in the world and have
      power to control people in the high place in the worldwide
      .Are you a business man or woman,artist, political,
      musician, student, do you want to be rich, famous, powerful
      in life, join the Illuminati brotherhood cult today and get
      instant rich sum of. 2 million dollars in a week, and a free
      home.any where you choose to live in this world
      BENEFITS GIVEN TO NEW MEMBERS of ILLUMINATI.
      1. A Cash Reward of USD $500,000 USD
      2. A New Sleek Dream CAR valued at USD $300,000 USD
      3.A Dream House bought in the country of your own choice
      4. One Month holiday (fully paid) to your dream tourist
      destination.
      5.One year Golf Membership package
      6.A V.I.P treatment in all Airports in the World 7.A total
      Lifestyle change 8.Access to Bohemian Grove
      account every month as a member
      9.One Month booked Appointment with Top 5 world
      Leaders and Top 5 Celebrities in the World.
      If you are interested of joining us in the great brotherhood of illuminati CONTACT MR ROLAND or WhatsApp him +2348142587627
      or email:illuminatipower666brotherhood@gmail.com

      Futa

  2. WELCOME TO THE GREAT BROTHERHOOD.
    Do you want to be a member of Illuminati as a brotherhood
    that will make you rich and famous in the world and have
    power to control people in the high place in the worldwide
    .Are you a business man or woman,artist, political,
    musician, student, do you want to be rich, famous, powerful
    in life, join the Illuminati brotherhood cult today and get
    instant rich sum of. 2 million dollars in a week, and a free
    home.any where you choose to live in this world
    BENEFITS GIVEN TO NEW MEMBERS of ILLUMINATI.
    1. A Cash Reward of USD $500,000 USD
    2. A New Sleek Dream CAR valued at USD $300,000 USD
    3.A Dream House bought in the country of your own choice
    4. One Month holiday (fully paid) to your dream tourist
    destination.
    5.One year Golf Membership package
    6.A V.I.P treatment in all Airports in the World 7.A total
    Lifestyle change 8.Access to Bohemian Grove
    account every month as a member
    9.One Month booked Appointment with Top 5 world
    Leaders and Top 5 Celebrities in the World.
    If you are interested of joining us in the great brotherhood of illuminati CONTACT MR ROLAND or WhatsApp him +2348142587627
    or email:illuminatipower666brotherhood@gmail.com

    JibuFuta