JINSI YA KULISHA NA KUTUNZA KUKU WA NYAMA  (BROILER) | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumanne, 8 Novemba 2016

JINSI YA KULISHA NA KUTUNZA KUKU WA NYAMA  (BROILER)

Image result for kuku wa nyama

Pole na majukumu ya hapa na pale ndugu yangu na tajiri mwenzangu. Karibu tena katika ukurasa wetu pemdwa kwa ajili ya kupata muongozo wa kufikia katika huu utajiri tunaousema. Leo nakuletea mada juu ya kulisha kuku wa nyama. Nakuomba usome ka uangalifu ili utoke na kitu.

Hapa nchini kwetu Tanzania kwa miaka ya hivi Karibuni watu wamejikita katika biashara ya Mifugo hasa ufugaji wa kuku wa kigeni na Leo hebu tuangalie lishe ya kuku wa nyama (Broilers).
Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri
a) Viinilisha vya wanga 60-65%
b) Protini 30-35%
c) Madini 2-8%
Pamoja na maji safi yenye mchanganyiko wa dawa ya vitamin.

Chakula cha vifaranga.
Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hutakiwa kuwa katika punje punje ndogo ndogo. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi. 

Aina ya vyakula Kiasi (kgs).
Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40Pumba za mtama au mahindi au uwele 27Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10Chumvi ya jikoni 0.5Virutubisho (Broiler premix)0.25 
JUMLA = 100kgs. 

Chakula cha kukuzia – growers mash.
Aina ya vyakula Kiasi (kgs).
Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25Pumba za mtama au mahindi au uwele 44Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 3.25Dagaa au mabaki ya samaki (fish meal) 10Chumvi ya jikoni 0.25Virutubisho (Broiler premix)0.5.
JUMLA = 100Kgs. 

Chakula cha kumalizia kukuzia (Growers finishers).
Aina ya vyakula Kiasi (kgs).
Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 31Pumba za mtama au mahindi au uwele 38
Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 18
Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25Dagaa au mabaki ya samaki (fish meal) 13Chumvi ya jikoni 0.5Virutubisho (Broiler premix)0.25.
JUMLA = 100Kgs. 


UTAMBUZI WA MAGONJWA  YA KUKU KUPITIA RANGI YA KINYESI.
1. MUHARO MWEUPE (pullorum bacilary diarrhoea)
ugonjwa huu huathiri zaidi vifaranga kabla ya wiki nne
huharisha mharo mweupe,
TIBA kuu ni usafi pekee kwenye banda na kuepusha maji yasimwagike ovyo.

2. KIPINDUPINDU CHA KUKU(fowl cholera)
kinyesi cha kuku ni njano
tumia dawa za salfa, eg Esb3 auamprollium

3COCCIDIOSIS
Mwanzo kinyesi cha kijivu na baadae huharisha damu iliyochanganyika
Tumia dawa ya VITACOX auANTICOX

4. MDONDO(Newcastle)
Kuku hunya kinyesi cha kijani lakini sio kila kijani ni newcastle. Dalili zingine ni pamoja na mabawa ya kuku kutanuka anakuwa kama amevaa koti. Ugonjwa huu hauna TIBA, zingatia ratiba ya chanjo tuu.

5. TYPHOID
Kinyesi cheupe
kinagandia sehemu za nyuma au hulowana sehemu za haja
dawa ni Esb3.

6. GUMBORO
Huathiri zaidi vifaranga
kinyesi huwa ni majimaji mepesi. Hauna Dawa.
tumia vitamini na antibiotic.

Kalenda ya chanjo kama ifuatavyo.
1week– Marek’s vaccine
2week– Newcastle vaccine
3week– Gumbolo vaccine
4week– Gumbolo vaccine tena
PUMZISHA CHANJO THEN ENDELEA IKIFIKA WIKI YA NANE
8week-Fowl pox vaccine
9week-Newcastle vaccine
PUMZIKA TENA MPAKA WIKI YA KUMI NA NAME
18week– Fowl typhoid vaccine
BAADA YA KUMALIZA CHANJO HIZI endelea kumpa chanjo ya Newcastle vaccine kila baada ya miezi mitatu au minne na kuzingatia hasa usafi wa banda na mazingira yanayozunguka. 
Ahsanteni 
Prepared by:
Marcodenis E. Misungwi. 
Assistance Agriculture Field Officer. 
0745896840

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT