Ugonjwa wa fangasi (Candidiasis) husababishwa na vimelea vijulikanavyo
kwa kitaalamu kama ‘Candida albicans’. Vimelea hivi hushambulia jinsia
zote lakini hushambulia zaidi wanawake sababu ya maumbile yao ya sehemu
za siri kuwa na unyevunyevu kitu kinachopelekea wao kuathiriwa zaidi
kuliko wanaume.
Watu karibu wote tunaishi na vimelea hivi katika miili yetu kwa kiwango
kidogo sana. Kinga ya mwili ikisaidiwa na bakteria wazuri wa mwili ndiyo
kupambana na vimelea hivi hata unaona huuguwi ila kinga ya mwili
ikiyumba kidogo na bakateria wabaya kuongezeka ndipo hapo unapokutana na
ugonjwa kamili.
Tatizo la kuwashwa sehemu za siri ni tatizo kwa watu wengi miaka ya sasa
na linawapata watu wa jinsia na rika zote yaani watoto, vijana hata
wazee.
Fangasi siyo sababu pekee ya kuwashwa sehemu za siri, kuna sababu na
magonjwa mengine yanahusika na tatizo hili na kupona au kuondoka kwa
sababu hizo ndiyo kupona kwa huo muwasho.
Sababu za muwasho sehemu za siri za mwanaume
Sababu zifuatazo zinaweza kuhusika na muwasho sehemu za siri kwa mwanaume:
Mzio au aleji
Maradhi ya fangasi
Ugonjwa wa upele
Chawa
Maambukizi ya bakteria
Magonjwa ya zinaa
Lishe duni
Baadhi ya dawa kutibu bakteria
Kushuka kwa kinga ya mwili
Kuambukizana toka mtu mmoja hadi mwingine kwa kuchangia nguo au vifaa
Hali ya hewa nayo yaweza kuwa chanzo hasa mazingira yenye joto sana
Sababu hizi ndizo hupelekea muwasho pia sehemu nyingine za mwili.
Dawa za asili zinazotibu fangasi kwa wanaume
Kumbuka kumuona daktari kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote, ni mhimu
kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi ikiwemo kubaini chanzo hasa cha
fangasi yako.
1. Mafuta ya habbat soda
Maambukizi ya fangasi yanatokea wakati bakteria wanapozidi juu ya ngozi
yako na kupelekea kutokea kwa magonjwa mengi ikiwemo miwasho, upele na
ukurutu. Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda ni mazuri kwa tiba
karibu kwa kila aina ya fangasi kitu kinachopelekea wanasayansi wengi
kuamini kuwa habbat soda ni dawa ya asili na mbadala mhimu zaidi kwa
kila mtu kuwa nayo nyumbani.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda
kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja. Mengine pakaa kama mafuta yako ya kupakaa
sehemu yenye muwasho kutwa mara 3 hadi 3
2. Mafuta ya nazi
Siyo sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na mafuta haya ya nazi
kama yanavyofanya mafuta mengine ya asili, kama unataka kuwa na ngozi
nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka
mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo
mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote
vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa
kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha.
3. Mu-aloe vera (mshubiri)
Ngozi hupenda sana Vitamini C na E ambazo zote zinapatikana katika aloe
vera na kusaidia kuboresha unene wa ngozi na kuiacha katika hali ya
umajimaji. Ikiwa utachanganya jeli ya aloe-vera na mafuta ya asili ya
nazi utapata krimu nzuri ya kuongezea viinilishe, mafuta mhimu na
unyevunyevu katika ngozi.
Jeli ya Aloe Vera hupenyeza katika ngozi kwa haraka mara nne zaidi ya
maji ya kawaida na sifa yake ya kulainisha ngozi husaidia ngozi kubaki
na unyevunyevu muda wote.
Mhimu: Pamoja na hizi dawa pia unahitaji kitu kitakachoimarisha kinga
yako ya mwili kwa ujumla na kwa sababu hii napendekeza utumie ama unga
wa majani ya mlonge au mbegu za maboga kila siku wakati ukiendelea na
hizi dawa za fangasi.
Pia hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku, jiweke msafi kila
mara na usishirikiane na wengine vitu kama taulo na vifaa vingine vya
kuogea.
Epuka vyakula vyenye sukari nyingi na hata sukari yenyewe ikibidi utumie
asali badala ya sukari kwenye kila unachohitaji sukari. Epuka pia
vyakula vya wanga.
Kama una ugonjwa wa kisukari jitibie kwanza kisukari.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT