Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Goodbless Lema amemshukuru Mbunge Lazaro
Nyalandu kwa kufanikisha safari ya Marekani ya watoto watatu ambao
walinusurika kifo katika ajali ya basi la shule ya Lucky Vicent
iliyotokea Karatu na kusababisha vifo vya watu 35.
Mh. Nyalandu alikuwa bega kwa bega na kufuatilia kila hatua kuhakikisha
watoto hao pamoja na wazazi wao na daktari wanasafiri kwenda nchini
Marekani kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.
"Mh Lazaro Nyalando , Mungu akubariki sana kwa kazi nzuri ya kusaidia
watoto waliopatwa na ajali hapa Arusha, jitihada zako Mungu atakulipa"
alisema Godbless Lema
Katika hatua nyingine Mh Lazalo Nyalandu ameomba pesa zitakazo endelea
kuchangwa na Watanzania na watu wengine duniani kwa ajili ya watoto hao
zitumike kujenga ICU katika hospitali ya Mount Meru.
"Kwa kuwa wadau wanaendelea kuchangia na kwa kuwa shule ya sekondari
zimekubali kuanzisha mfuko ambao wanausimamia wenyewe na kwa kuwa mfuko
huo lengo lao kubwa lilikuwa kuwasafirisha hawa watoto kazi ambayo
imefanywa na Samaritan Purse lakini lengo la pili ilikuwa ni kwenda
kuwatibu kazi ambayo inafanywa na Shirika la STEMM kwa kushirikiana na
Hospitali kuu ya Mercy hivyo kazi itakayobaki Mh Mkuu wa Mkoa itakuwa
ndogo, kwa hiyo nimeomba na nimeshaurina nao na wamekubali kwamba
Watanzania na wanadunia wote watakao endelea kuchanga fedha zote ziletwe
kwako Mh Mkuu wa mkoa ili ziweze kujenga kituo cha wagonjwa ambao
wanahitaji huduma ya haraka (ICU) katika hospitali yetu ya Mount Meru" alisema Nyalandu
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT