Katika post hii utajifunza vyakula mbalimbali ambavyo wanaume hawatakiwi
kula ili kubaki na afya bora wakati wote. Kuna vingine unaweza kuwa
unavitumia kila siku bila mwenyewe kujuwa.
1. Punguza kula vyakula feki kuzuia kupoteza nywele
Moja ya matatizo makubwa upande wa urembo kwa wanaume ni kupoteza nywele
(upala). Lakini kama unatafuta kitu cha kukilaumu dhidi ya tatizo lako
la kunyonyoka nywele basi ni hiyo sahani yako ya chipsi unayokula kila
siku. Vyakula feki (junk foods) ni hivyo vinapatikana kwenye fast foods
na takeaway centers nyingi hasa mijini kadharika vyakula vile vyote vya
kwenye maboksi.
Vyakula hivi feki vina kiasi kingi mno cha lehemu (cholesterol) na
lehemu hii hupelekea kile huitwa kwa kitaalamu kama ‘pregnenolone’ na
kupelekea kiasi kikubwa cha ‘dihydrotestosterone’ (DHT) na hatimaye
kupotea kwa nywele kichwani a.k.a upara.
Kunyonyoka kwa nywele kunaweza kuwa ni jambo la kurithi (genetics)
lakini vile vile aina ya chakula unachokula kinaweza kuwa kinahusika
moja kwa moja.
2. Punguza kunywa pombe au acha kabisa kuzuia kuota matiti
Wanaume wengi wanaokunywa bia kupita kiasi huwa na uwezekano mkubwa wa
kupatwa na tatizo la kuota matiti kama wamama tatizo lijulikanalo kwa
kitaalamu kama ‘gynecomastia’.
Kwenye bia au pombe mara nyingi hakuna lishe ya moja kwa moja na hivyo
hukufanya ujisikie njaa au hata kuongzeka kwa njaa zaidi na ndiyo sababu
unaambiwa kama huna uhakika utakula wapi ni bora usinywe pombe ili
kulinda afya yako.
Kwenye bia kuna kitu kama homoni ya oestrogen ya kupandikizwa na hivyo
unywaji pombe kupita kiasi kuna uhusiano wa moja kwa moja na matokeo ya
wanaume kuwa na matiti kama wanawake.
3. Acha kutumia mafuta ya mboga mboga kuepuka saratani ya tezi dume
Mafuta yatokanayo na mboga mboga au mimea yamekuwa yakipigiwa debe kwa
miaka mingi na watu wanaojihusisha na lishe na wale wenye hasira sana na
mafuta yatokanayo na wanyama. Hata hivyo leo nakujulisha mafuta hayo si
salama sana kutumika na mwanaume kila siku. Hili limekuja hasa kutokana
na kuongezeka kwa magonjwa ya moyo na lehemu na watu wakahimizwa
kutumia mafuta ya namna hiyo.
Lakini mafuta haya ya mboga mboga ndiyo kitu kibovu kabisa unatakiwa
kukiepuka ili usipatwe na saratani ya tezi dume. Linapokuja suala la
kujilinda saratani ya tezi dume basi mafuta yenye omega 3 ndiyo
suluhisho la kudumu na siyo omega 6 kama ilivyo kwenye vyakula vingi vya
kwenye makopo, mafuta ya alizeti, maharage ya soya, mafuta ya canola
na mafuta ya corn na mengine yote yenye omega 6.
4. Popcorn
Popcorn au bisi ni chakula kingine mwanaume hatakiwi kula, hupikwa kwa
kutumia mafuta yasiyo na afya, sodiamu nyingi na ni chanzo cha baadhi ya
kansa. Kuna kitu kinaitwa ‘Diacetyl’ kinachopatikana kwenye popcorn
ambacho kinahusika na kusababisha kansa na kuna kingine kiitwacho
‘Perfluorochemicals’ ambacho huathiri tezi ya thyroid na ugonjwa wakati
huo huo husababisha ugonjwa wa kupungukiwa umakini ujulikanao kwa
kiingereza kama ‘Attention-deficit/hyperactivity disorder (ADHD)‘.
Ni vizuri kuacha kula popcorn
5. Mkate mweupe
Mkate mweupe una wanga mwingi zaidi usio na faida. Kwenye hatua za
kutengeneza mkate mweupe vitamini zote za kundi B hupotea, hupotea pia
nyuzinyuzi (fiber). Siyo hivyo tu mkate mweupe umesemekana kuwa ni
sababu ya ugonjwa wa kisukari na kuongeza uzito zaidi mwilini wakati huo
huo ukisababisha tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.
Vingine vinavyofanana na na hilo ni ugali wa sembe, tambi nyeupe, chai ya rangi na kahawa.
Kula mkate ambao ngano yake haikukobolewa (brown bread), kula ugali wa
dona na chai unaweza kutumia tangawizi au mdalasini badala ya majani ya
chai.
6. Chumvi ya mezani
Chumvi ya mezani ile ya unga nyeupe haifai kwa mwanaume. Kila mmoja
amesikia chumvi hii husababisha shinikizo la juu la damu na pamoja na
hayo bado sehemu kubwa ya watu wanatumia chumvi hii.
Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini madini na hupitishwa
katika joto la nyuzi joto 1093. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40
ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile
‘aluminium silicate’ huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki
katika hali ya unga. Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo
wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha
ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijapita kiwandani (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi kwa afya ya mwanaume.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT