Ndizi zina virutubisho vingi kama vile vitamini, nyuzinyuzi, protini,
wanga, madini ya chuma na virutubisho vya sukari kama ‘Sucrose’ na
‘Fructose’. Wataalam wa lishe wanasema kula ndizi mbili kwa siku kwa
muda wa mwezi tu, afya yako itaimalika.
Kuondokana na tatizo la Kiungulia
Ndizi kiasili sio tunda lenye asidi kwa wingi, ikumbukwe kuwa kiungulia
husababishwa na uwepo wa asidi nyingi mwilini. Hivyo ndizi ni tiba kwa
wote ambao wanasumbuliwa na kiungulia. Kula japo ndizi moja kwa siku
basi itatuliza haraka na kuondoa dalili zote za kiungulia.
Kuondoa Presha
Ndizi pia zina wingi wa madini ya ‘Sodiam’ na ‘Potassium’ ambayo huweka
sawa presha ya damu na kuimarisha afya ya moyo. Madini hayo pia husaidia
kutanua misuli ya moyo ili kufanya kazi zake kwa urahisi.
Kuongeza Nguvu
Endapo utakula ndizi mbili kabla ya kazi yoyote hakika nguvu zako
zitaongezeka. Kama ilivyoelezwa awali ndizi zina vitamini, madini,
wanga, na ‘Glycemic’ (kiwango cha sukari yenye kutia nguvu mwilini)
ambavyo vyote hivyo ni vyanzo vizuri vya kutia nguvu mwilini kwa haraka.
Kuondokana naugonjwa wa Vidonda vya tumbo
Ndizi zina mchanganyiko wa vilainishi na nyuzinyuzi ambazo hulainisha
tumbo na kupelekea kuzuia mikwaruzo kwenye utumbo hivyo kuzuia vidonda
vya tumbo.
Husaidia wagonjwa wa Anaemia
Anaemia kitaalamu ni ugonjwa unaosababishwa na upungufu wa madini ya
chuma mwilini, madini hayo husaidia kwenye uzalishaji wa chembechembe za
damu nyekukundu ambazo huhitajika kwa wingi mwilini.
Ndizi zina madini ya chuma ambayo huwasaidia wagonjwa wa Anaemia kwa
sababu madini ya chuma husukuma uzalishaji wa ‘Haemoglobin’. Hivyo
huongeza chembechembe nyekundu za damu na kuongeza mzunguko wa damu
mwilini.
Haemoglobin ni protini inayopatikana kwenye chembechembe nyekundu za
damu ambazo husafirisha hewa ya Oksijeni kutoka kwenye mapafu na kwenda
sehem mbalimbali za mwili, Aidha huchukua pia hewa ya Kabondayoksaidi
kutoka kwenye viungo vya mwili na kurudisha kwenye mapafu.
Wakati mwengine ugonjwa wa Anaemia hujulikana kama Upungufu/Ukosefu wa damu mwilini.
Huondoa mgandamizo wa mawazo
Ndizi zina muunganiko wa pekee ambao kitaalam huitwa ‘Tryptophan’ hii ni
asidi inayopatikana kwenye protini, ambayo husaidia kwa kutotokea
mgandamizo wa mawazo. Virutubisho hivi vikiingia mwilini vinabadirika na
kuwa ‘Serotonin’ ambayo hupatikana moja kwa moja kwenye ubongo, huweka
misuli sawa na husaidia mtu ajisikie furaha na kuondokana na mawazo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT