Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na
Mazingira, January Makamba wiki hii alitembelea ofisi za WCB na
kuonyeshwa mambo mbalimbali ambayo yanafanyika katika kila kitengo.

Akiongea katika utambulisho huo, Babu Tale alisema wao katika usambazaji
wa kazi za wasanii wao huanza kwa watu wa chini ambao wanapatikana
mtaani.

“Hii ni ofisi ya watu wa creative,” alisema Tale katika ubambulisho huo.
“Wakati wa kutoa nyimbo mpya lazima tunakaa na kuwaza tunafanya nini na
tutatoa kwa style gani ili tuanze kuukamata mtaa tunafanyaje kuhusu
mtaa. Kwa hiyo tunapotoa nyimbo tunahakikisha kila mtu mtaani anayo
halafu ndio tunaiachia redioni. Kwahiyo ikienda redioni watu wa mtaa
watakuwa wanaisukuma ile ya redio,”
Pia Diamond alisema wanaitegemea mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa katika kusambaza nyimbo zake kwa uharaka zaidi.
Kwa upande wa Waziri January Makamba alimmwagia sifa Diamond pamoja na team yake kwa kufanya kazi nzuri.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT