Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Bulimba
Jeshi la polisi nchini limesema halipendelei chama chochote cha
siasa nchini na badala yake linachofanya ni kutoa ulinzi wa kuhakikisha
usalama wa raia na mali zao upo wakati wote.
“Jeshi la polisi halina upendeleo kwa chama chochote cha siasa nchini, ndiyo maana kila chama kikizingatia kanuni za kuomba mikutano ya hadhara kinapata ulinzi kutoka jeshi la polisi, hivyo kazi yetu kubwa ni kuhakikisha usalama wa raia na mali zao upo, hivyo tukizuia mkutano wowote ni kwa lengo la kudumisha usalama wa raia na mali zao na kupafanya Tanzania kuwa sehemu salama ya nchi."
Aidha Jeshi la polisi limewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa ambazo zitasaidia kuimarisha ulinzi na usalama na taarifa watakazotoa zitachukuliwa maanani na kufanyiwa kazi mara moja, na namba za kutumika ni 111 au 112.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

0 comments:
POST A COMMENT