Msanii Darasa ambaye amerudi kwa nguvu zote kwenye game ya hip hop ya
bongo, amesema suala la wasanii wa sasa kusema wanafanya muziki wa
biashara na siyo ule muziki unaoishi, wanakuwa wanakosea.
Darasa
Darasa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na EATV, na kusema msanii
mzuri ni yule anayefanya muziki mzuri na kuacha ujiuze wenyewe kwenye
biashara.
“Ni tatizo kubwa sana kwa msanii ambaye anasikika anasema hivyo mbele
ya mashabiki au mbele ya mdau, kuna biashara siyo lazima umwambie mtu
mi nafanya biashara hata kama unataka kufanya biashara, kwanza lazima
ujali feelings, tunatengeneza muziki kwa ajili ya watu na naamini maisha
yetu yanakuja kutegemea hivyo, wale watu watacare baada ya wewe
kuwatengenezea production nzuri”, alisema Darasa.
Darasa aliendelea kusema kwa upande wake yeye anafanya muziki mzuri na
ndiyo maana ameweza kukaa kwenye game kwa muda mrefu na kurudi kwa
heshima kubwa.
“Mi nafanya muziki mzuri ndiyo maana sijawahi kusikika nikimwambia
mtu nafanya biashara, nime'change' game yangu natengeneza muziki mzuri
ambao unawafaa watu wangu, najua wao wata'care, nitaifanya sanaa yangu
kuwa sehemu nzuri ya kuishi kwa mashabiki mpaka mimi mwenyewe”, alisema Darasa.
Kuhusu kufanya muziki kama biashara msanii Diamond Platnumz amesikika akiliongea sana kwa nyakati tofauti tofauti
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT