Unaweza kushangazwa na hii, mtu aliyekufa kuongoza list ya
mastaa wanaingiza pesa nyingi wakati hawapo duniani. Michael Jackson ni
mmoja wa mastaa ambao vifo vyao vimechukua headlines tena baada
ya Forbes kumtaja kuingiza pesa nyingi zaidi baada ya kifo chake.
Mfalme
wa zamani wa muziki wa Pop, Michael Jackson aliyefariki dunia miaka 7
iliyopita bado ameendelea kuingiza pesa nyingi kiasi cha dola za
Marekani milioni 825 mwaka 2016, na kushika nafasi ya kwanza kama star
aliyekufa na anayeingiza pesa nyingi zaidi.
Kwa
mujibu Forbes, kilichomfanya MJ kuingiza mkwanja mrefu zaidi hata baada
ya kifo chake ni baada ya kuamua kuuza hisa zake za sanaa kwenye
kampuni ya Sony kwa dola za Marekani milioni 750.
Star huyo
wa hit single ya Thriller alinunua hisa za kampuni ya muziki ya Fab Four
mwaka 1984 kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 47.5 na kisha kuuza
asilimia 50 ya hisa zake kwa kampuni ya Sony mwaka 1995 kwa dola
milioni 115.
Mastaa waliotajwa kweny list hiyi ni hawa hapa.
1: Michael Jackson – $825 million
3: Golfer Arnold Palmer – $40 million
4: Elvis Presley – $27 million
5: Prince – $25 million
6: Bob Marley -$21 million
7: Theodor ‘Dr. Seuss’ Geisel – $20 million
8: John Lennon – $12 million
9: Physicist Albert Einstein – $11.5 million
10: Original pin-up girl Bettie Page – $11 million
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT