Bepari Classic: MICHEZO
Breaking News
Loading...
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MICHEZO. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MICHEZO. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 16 Oktoba 2016

Mbwana Samatta Atajwa Tuzo ya Mchezaji Bora ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya GENK ya nchini Ubelgiji ametajwa miongoni mwa wachezaji 30 wanaowani Tuzo ya Mchezaji Bora ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

Wachezaji wengine ni pamoja na Mkenya Victor Wanyama anayecheza ligi kuu ya Uingereza katika klabu ya Tottenham Hotspur, Denis Onyango kutoka Uganda anayekipiga katika klabu ya Mamelodi Sundowns.

Hapa chini ni orodha kamili.

1. Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)

2. El Arabi Hillel Soudani (Algeria & Dinamo Zagreb)

3. Islam Slimani (Algeria & Leicester City)

4. Samuel Eto’o (Cameroon & Antalyaspor)

5. Benjamin Mounkandjo (Cameroon & Lorient)

6. Serge Aurier (Cote d’Ivoire & PSG)

7. Eric Bailly (Cote d’Ivoire & Manchester City)

8. Yao Kouasi Gervais ‘Gervinho’ (Cote d’Ivoire & Hebei Fortune)

9. Mohamed Salah (Egypt & Roma)

10. Mohamed El Neny (Egypt & Arsenal)

11. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Dortmund)

12. Andre Ayew (Ghana & West Ham)

13. Victor Wanyama (Kenya & Tottenham)

14. William Jebor (Liberia & Wydad Athletic Club)

15. Mehdi Benatia (Morocco & Juventus)

16. Hakim Ziyech (Morocco & Ajax)

17. John Mikel Obi (Nigeria & Chelsea)

18. Kelechi Iheanacho (Nigeria & Manchester City)

19. Ahmed Musa (Nigeria & Leicester City)

20. Cedric Bakambu (DR Congo & Villareal)

21. Yannick Bolasie (DR Congo & Everton)

22. Sadio Mane (Senegal & Liverpool)

23. Kalidou Koulibaly (Senegal & Napoli)

24. Keegan Dolly (South Africa & Mamelodi Sundowns)

25. Itumeleng Khune (South Africa & Kaizer Chiefs)

26. Mbwana Samatta (Tanzania & Genk)

27. Aymen Abdennour Tunisia & Valencia)

28. Wahbi Khazri (Tunisia & Sunderland)

29. Dennis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)

30. Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns)

Alhamisi, 13 Oktoba 2016

Michezo TOP10: Wachezaji wanaoongoza kwa mauzo ya jezi England msimu wa 2016/2017

List ya mastaa 10 wa soka wa Ligi Kuu England ambao wanaongoza katika list ya mastaa wa EPL wanofanya vizuri katika mauzo ya jezi, list hiyo imeongozwa na kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Man United Paul Pogba ambaye ndio mchezaji ghali zaidi duniani.
Mastaa wengine waliofanikiwa kuingia katika list hiyo ni Zlatan Ibrahimovic ambaye alijiunga na Man United kama mchezaji huru akitokea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.
1- Paul Pogba – Man United
2- Zlatan Ibrahimovic Man United
3- Alex Sanchez- Arsenal
4-Mesut Ozil – Arsenal
5- Coutinho – Liverpool
6- David de Gea – Man United
7- Sadio Mane – Liverpool
8- Dimitri Payet-West Ham United
9- Eden Hazard – Chelsea
10 – Marcus Rashford – Man United

Pogba: Napenda kocha Jose Mourinho anichezeshe mbele zaidi

Mchezaji ghali zaidi kwasasa duniani kiungo Paul Pogba amesema kuwa anapenda kocha Jose Mourinho amchezeshe mbele zaidi katika kikosi cha Man United.

Tangu aliporejee katika klabu ya Manchester United kwa pauni milioni 89, Pogba amekuwa akichezeshwa chini zaidi katika sehemu ya kiungo, akifanya majukumu ya ulinzi.

Amesema kuwa kuchezeshwa chini zaidi katika sehemu ya kiungo katika klabu ya Man United, kuna mgharimu sana.

Katika mechi ya Ufaransa dhidi ya Uholanzi baada ya kucheza juu zaidi kwenye sehemu ya kiungo katika mechi ya jumatatu hii iliyopita, kiungo huyo alionesha uwezo mkubwa na kufunga goli zuri ambalo liliipa timu yake pointi 3.

“Ninajitahidi kuzoea,” Paul alisema hayo wakati akiongea na Manchester Evening News.

“Mimi ni mchezaji ninayependa kwenda mbele. Kocha ananipa maelekezo najaribu kuyafuata. Inabidi nirudishe mipira na kufanya majukumu ya ulinzi.

‘Inanigharimu sana kucheza tofauti, kama vile achezavyo Andrea Pirlo.’

Jumatano, 12 Oktoba 2016

Omog awatwishwa zigo Mavugo na Ajibu

Tokeo la picha la mavugo simba s.c

Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, amewataka washambuliaji wake, Laudit Mavugo na Ibrahim Ajibu kuhakikisha wanaiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi dhidi ya Mbeya City, leo.

Kocha huyo amesema wachezaji hao wanatakiwa kuhakikisha wanafanya kama kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Shiza Kichuya alivyofanya kwenye mchezo dhidi ya Azam na Yanga.

Leo jioni timu hizo mbili zinashuka uwanjani katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ambapo Simba itakuwa ikihitaji ushindi ili izidi kujichimbia juu katika msimamo wa ligi hiyo wakati Mbeya City nayo inahitaji matokeo mazuri ili iweze kujitengezea mazingira mazuri kwenye ligi hiyo.

Omog alisema kuwa ufanisi mzuri wa Mavugo na Ajibu ambao wamekuwa wakiuonyesha mazoezini katika kuzifumania nyavu hivi karibuni, wanatakiwa kuuonyesha uwanjani leo kama ambavyo Kichuya amekuwa akifanya kwa sababu wao ndiyo washambuliaji anaowategemea kwa kufunga.

Katika mechi mbili zilizokuwa na ushindani mkubwa ambazo Simba ilicheza hivi karibuni dhidi ya Azam na Yanga, Kichuya ndiye mchezaji aliyeifungia timu hiyo mabao ambayo yaliwezesha kujikusanyia pointi tatu kwenye mechi hizo ambazo Ajibu na Mavugo walishindwa kuonyesha makeke yao.

“Namshukuru Mungu mpaka sasa hakuna majeruhi yeyote katika kikosi changu, wachezaji wote wapo vizuri ila nimewaambia kuwa nataka ushindi katika mchezo huu.
“Mavugo na Ajibu pia nimewaambia wapambane vilivyo kuhakikisha tunashinda kwa sababu wao ndiyo washambuliaji tunaowategemea.

“Nafikiri wanatakiwa kuonyesha kasi nzuri sana kwenye mchezo huu,” alisema Omog.

SOURCE: CHAMPIONI

Hatma ya ukodishwaji Yanga Oktoba 23

Dar es Salaam. Wakati mjadala wa kukodishwa Yanga kwa miaka 10 ukishika kasi, uongozi wa klabu hiyo umesema uamuzi wa mwisho utatolewa  kwenye mkutano mkuu wa Oktoba 23.

Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema mkutano mkuu wa Oktoba 23 ndiyo utaamua hatima ya kukodishwa kwa klabu hiyo au la.

“Ajenda ya kukodisha klabu itapitishwa na mkutano mkuu ujao, akidi ikitimia kwa mujibu wa katiba yetu zoezi hilo litafanyika,” alisema Baraka na kufafanua.

“Yanga ‘inadili’ na wanachama wanaolipia kadi zao, wapo wenye kadi, lakini hawazilipii hao siwezi kuwazungumzia kwa sababu si wanachama hai.

“Ukizungumzia wanachama wa Yanga kiukweli ni wengi, ni zaidi ya 10,000, lakini wote hao si ‘active’ (hai).

Katibu huyo alisema mkutano mkuu wa dharura uliopita ulikuwa na wanachama 1,800 wanaolipia ada ya kadi zao za uanachama.

“Mambo mengine ni ya kiofisi, hayapaswi kutangazwa, lakini mkutano wetu mkuu wa dharura uliopita ulikuwa na wanachama 1,800 waliokuwa hai,” aliongeza Baraka.

Jumanne, 11 Oktoba 2016

Griezmann amsikitikia Pogba kupitia kipindi kigumu Man Utd

 

Paris, Ufaransa. Mshambuliaji wa Ufaransa, Antoine Griezmann ameeleza kusikitishwa na kiungo wao, Paul Pogba akisema anahitaji kusaidiwa, kupendwa zaidi kipindi hiki anachokabiliwa na wakati mgumu.

Kauli hiyo ya Griezmann ameitoa baada ya Ufaransa kuilaza Bulgaria kwa mabao 4-1 kwenye mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia ambako Pogba alicheza vizuri, ingawa si kwa kiwango chake cha kawaida.

Alieleza kuwa Pogba anahitaji kuonyeshwa mapenzi ili aweze kurejesha kiwango cha ubora ambacho kimeporomoka kwa kiasi kikubwa.

Kikosi cha Ufaransa, Les Bleus kilirejea uwanjani hapo, Stade de France kwa mara ya kwanza tangu kidunguliwe na Ureno kwa bao la dakika za nyongeza kwenye fainali za Ulaya, Euro 2016, usiku ambao Pogba alikumbwa na jinamizi la kupotea kwa kiwango chake.

Kijana huyo mwenye miaka 23 amekuwa na wakati mgumu tangu atue Manchester United kwa ada ya uhamisho ya karibu Pauni 100 milioni akitokea Juventus na kupewa jukumu kubwa kwenye klabu hiyo mpya, jambo ambalo Griezmann anasisitiza ndilo linalomtesa.

Akizungumza na gazeti la L’Equipe baada ya mchezo huo, Griezmann alisema: “Pogba anahitaji kupendwa zaidi arejeshe kiwango chake. “Anacheza mchezo tofauti na uliozoeleka akiwa Juve, sasa Manchester ni timu tofauti, pia kikosi cha Ufaransa ni tofauti kabisa kimfumo,” aliongeza.

Griezmann, mshindi wa kiatu cha dhahabu kwa mabao Euro 2016 na tuzo ya mchezaji bora aliifungia mojawapo ya mabao manne nchi yake, alitengeneza jingine kwa mwenzake wa Atletico Madrid, Kevin Gameiro aliyefunga mawili.

Gamiero aling’ara katika mchezo huo wa kwanza kwenye kikosi cha Ufaransa kwa miaka mitano ambako alifurahia kushirikiana na mwenzake, Griezmann. Pia, kocha Dideir Deschamps alikuwa mwenye furaha kutokana na ushirikiano huo.

Akizungumza na gazeti la L’Equipe baada ya mchezo huo, Griezmann alisema: “Pogba anahitaji kupendwa zaidi arejeshe kiwango chake. “Anacheza mchezo tofauti na uliozoeleka akiwa Juve, sasa Manchester ni timu tofauti, pia kikosi cha Ufaransa ni tofauti kabisa kimfumo.”

Jumatatu, 10 Oktoba 2016

TOP 5: Wachezaji bora wa Laliga katika historia, Ronaldo hayumo hata Top 20

Moja kati ya habari zinazo-trend katika soka leo October 9 2016 ni kuhusiana na list ya wachezaji bora wa muda wote wa LaLiga, kituo cha uchunguzi, histoaria na takwimu za soka Hispania  (CIHEFE) kimetaja majina ya wachezaji bora wa muda wote katika historia ya LaLiga.
Licha ya kuwa utafiti huo wa CIHEFE uliotaja list hiyo kuanza kuleta minong’ono katika mitandao, wengi wameshangazwa kuona mshindi wa tuzo tatu za Ballon d’Or Cristiano Ronaldo kuwekwa namba 23 na mpinzani wake wa karibu katika soka Lionel Messi wa FC Barcelona kupewa nafasi ya nne.
adaa
Namba moja ya list hiyo amepewa Raul Gonzalez mkongwe wa zamani wa Real Madrid, mkongwe Cesar Rodriguez yupo namba 2, Telmo Zarra namba tatu, Lionel Messi nafasi ya nne na Enrique Castro ‘Quini’ nafasi ya tano, wachezaji kama David Villa yupo nafasi ya 32, Xavi nafasi ya 49 wakati Iker Casillas ameshika nafasi ya 62.
Imetajwa List ya wachezaji bora wa Laliga wa muda wote, Raul namba 1, Messi namba 4 wakati Cristiano Ronaldo yupo namba 23 #CIHEFE pic.twitter.com/GEOSGWO7Ha

Jumatatu, 3 Oktoba 2016

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA MZUMBE UNIVERSITY MASTERS 2016/2017

 Tokeo la picha la MZUMBE.AC.TZ

Kindly open link below to view candidates selected in Master programmes 2016/2017 phase one

https://drive.google.com/…/fo…/0B9Vd59-UZpsjQnhsWVlHaURBV0U…