Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema mkutano mkuu wa Oktoba 23 ndiyo utaamua hatima ya kukodishwa kwa klabu hiyo au la.
“Ajenda ya kukodisha klabu itapitishwa na mkutano mkuu ujao, akidi ikitimia kwa mujibu wa katiba yetu zoezi hilo litafanyika,” alisema Baraka na kufafanua.
“Yanga ‘inadili’ na wanachama wanaolipia kadi zao, wapo wenye kadi, lakini hawazilipii hao siwezi kuwazungumzia kwa sababu si wanachama hai.
“Ukizungumzia wanachama wa Yanga kiukweli ni wengi, ni zaidi ya 10,000, lakini wote hao si ‘active’ (hai).
Katibu huyo alisema mkutano mkuu wa dharura uliopita ulikuwa na wanachama 1,800 wanaolipia ada ya kadi zao za uanachama.
“Mambo mengine ni ya kiofisi, hayapaswi kutangazwa, lakini mkutano wetu mkuu wa dharura uliopita ulikuwa na wanachama 1,800 waliokuwa hai,” aliongeza Baraka.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

0 comments:
POST A COMMENT