Kocha
Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, amewataka washambuliaji wake,
Laudit Mavugo na Ibrahim Ajibu kuhakikisha wanaiwezesha timu hiyo
kuibuka na ushindi dhidi ya Mbeya City, leo.
Kocha
huyo amesema wachezaji hao wanatakiwa kuhakikisha wanafanya kama kiungo
mshambuliaji wa timu hiyo Shiza Kichuya alivyofanya kwenye mchezo dhidi
ya Azam na Yanga.
Leo
jioni timu hizo mbili zinashuka uwanjani katika mchezo wa Ligi Kuu Bara
kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ambapo Simba itakuwa ikihitaji
ushindi ili izidi kujichimbia juu katika msimamo wa ligi hiyo wakati
Mbeya City nayo inahitaji matokeo mazuri ili iweze kujitengezea
mazingira mazuri kwenye ligi hiyo.
Omog
alisema kuwa ufanisi mzuri wa Mavugo na Ajibu ambao wamekuwa
wakiuonyesha mazoezini katika kuzifumania nyavu hivi karibuni,
wanatakiwa kuuonyesha uwanjani leo kama ambavyo Kichuya amekuwa akifanya
kwa sababu wao ndiyo washambuliaji anaowategemea kwa kufunga.
Katika
mechi mbili zilizokuwa na ushindani mkubwa ambazo Simba ilicheza hivi
karibuni dhidi ya Azam na Yanga, Kichuya ndiye mchezaji aliyeifungia
timu hiyo mabao ambayo yaliwezesha kujikusanyia pointi tatu kwenye mechi
hizo ambazo Ajibu na Mavugo walishindwa kuonyesha makeke yao.
“Namshukuru
Mungu mpaka sasa hakuna majeruhi yeyote katika kikosi changu, wachezaji
wote wapo vizuri ila nimewaambia kuwa nataka ushindi katika mchezo huu.
“Mavugo na Ajibu pia nimewaambia wapambane vilivyo kuhakikisha tunashinda kwa sababu wao ndiyo washambuliaji tunaowategemea.
“Nafikiri wanatakiwa kuonyesha kasi nzuri sana kwenye mchezo huu,” alisema Omog.
SOURCE: CHAMPIONI
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT