Mahakama moja nchini Saudi Arabia imewapa hukumu ya kifo watu 15 kwa
kuwa majasusi wa Iran.Watu hao ni miongoni mwa 32 ambao wanatoka
madhehebu ya Ki-Shia, akiwemo raia mmoja wa Iran na Afghanistan.
Wakuu wa mashtaka wamewalaumu kwa kufanya njama ya mapinduzi ambapo pia
wametuhumiwa kwa kuwa na mtandao wa ujasusi kwa ushirikiano na Iran na
kutoa taarifa muhimu kuhusu jeshi.
Taharuki imeendelea kati ya Saudi Arabia inayofuata madhehebu ya
Ki-Sunni na Iran inayofuata imani ya Shia. Ufalme wa Saudia ulikata
uhusiano wa kidoplomasia na Iran baada ya waandamanaji kuvamia ubalozi
wake mjini Tehran kulalamikia kunyongwa kwa muhubiri maarufu wa Kishia
raia wa Saudi Arabia Sheikh Nimr al-Nimr.
Saudia ilisisitiza kwamba Nimr alikua na makosa ya ugaidi, lakini
kiongozi mkuu wa Iran akasema alinyongwa kwa kuukosoa ufalme. Dola hizi
mbili pia zinaunga mkono makundi pinzani katika vita nchini Yemen. Raia
Wa-Shia ni asili mia 10 pekee nchini Saudi Arabia na wamekua
wakilalamikia kubaguliwa katika elimu ya umma, uhuru wa kuabudu, nafasi
za kazi na hata masuala ya haki.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT