Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls amejiuzulu wadhifa wake, ili
kujikita katika kampeni za kuwania urais katika uchaguzi utakaofanyika
Mei mwaka ujao. Waziri wa mambo ya ndani, Bernard Cazeneuve, ameteuliwa
kuwa waziri mkuu mpya.
Valls amejiuzulu siku moja baada ya kutangaza nia yake ya kugombea
urais, baada ya Rais Francois Hollande kuamua kutogombea muhula wa pili
kwa tiketi ya chama chao cha kisoshalisti.
0 comments:
POST A COMMENT