Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitembelea ujenzi wa
hospitali hiyo leo jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda amesema ndoto ya mama mmoja kitanda kimoja itatimia endapo
ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto inayojengwa Chanika kwa ushirikiano
wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini na Mkoa wa Dar es Salaam
utakamilika.
Makonda alisema ujenzi wa hospitali hiyo ni muda mwafaka kwa wanawake na watoto kuwa na uhakika wa kupata huduma ya afya.
Alisema hospitali hiyo inayojengwa itahudumia watu 1000 wa nje huku
vitanda katika hospitali hiyo ni 160 kwa ajili ya akina mama na watoto.
Aidha alisema wananchi waendelelee kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John
Pombe Magufuli ya ulipaji kodi ili nchi iwe na uwezo hata kusaidia nchi
nyingine kama wanavyofanya wa Korea.
Makonda alisema madaktari watakao kwenda katika hospitali hiyo watakuwa
na makazi humo ili kuondoa usumbufu wa kusafiri kila siku.
Alisema serikali inawapenda wananchi wake kuhakikisha wanapata huduma ya afya bora hususani wanawake na watoto.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT