Kiama chaikumba TASAF, maafisa 111 watumbuliwa | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumanne, 6 Desemba 2016

Kiama chaikumba TASAF, maafisa 111 watumbuliwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF) kuwasimamisha kazi mara moja maafisa ushauri na mipango 106 katika ngazi ya halmashauri nchini.

Wengine wanaopaswa kusimamishwa ni pamoja na maafisa 5 wa ngazi za juu wa makao makuu ya TASAF.

Maafisa hao wanaondolewa kazini mara baada ya kuingiza kaya zisizo na sifa ya kupokea ruzuku serikalini na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 6.4.

Jambo hilo limemlazima Mhe. Kairuki kuamuru wachunguzwe ndani ya mwezi mmoja huku Meneja na Mkurugenzi wa Uratibu pamoja na maafisa watano waandamizi wa makao makuu ya TASAF nao wakisimamishwa kazi.

Mhe. Kairuki amesema asilimia 28.2 ya watanzania wote ni masikini sana na kwamba serikali imekwisha kutumia zaidi ya shilingi bilioni 391 kwa ajili ya kuhudumia awamu ya tatu ya mpango wa kunusuru kaya masikini na kwa sasa inajikita kuhakikisha kuwa wanaonufaika na ruzuku hiyo ni walengwa pekee.


Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT