Kiharusi
ni ugonjwa ambao huathiri ubongo na ufanyaji kazi wake. Hujulikana kama
stroke au brain attack kwa Kiingereza. Unapopata kiharusi, seli za
sehemu fulani za ubongo hushidwa kufanya kazi kutokana na damu kushindwa
kufika kwenye seli hizo za ubongo. Kiharusi huweza kuathiri sehemu
yoyote ya ubongo, na hivyo kuathiri ufanyaji wa shughuli za kila siku za
mgonjwa.
Ugonjwa huu ni hatari na mara
nyingi hujitokeza ghafla, ingawa wakati mwingine kuna dalili unazoweza
kupata kuashiria ugonjwa huu. Dalili hutegemea na sehemu ya ubongo
iliyoathirika. Sehemu kubwa ya ubongo ikiathirika huweza kusababisha mtu
kushindwa kuongea, kujitambua na wengi hushindwa kurudi hali zao za
kawaida.
Huu ni ugonjwa hatari ambao unaweza
kusababisha mtu kupoteza maisha ghafla. Hivyo ni muhimu sana kuwahi
hospitali kwa ajili ya matibabu. Pamoja na matibabu mazuri, kuna
uwezekano mgonjwa akapata ulemavu wa maisha kutokana na kiharusi.
Uwezekano wa kupata kiharusi huongezeka kadri umri unavyoenda.
NAMNA KIHARUSI KINAVYOTOKEA
Ili kufanya kazi zake, seli za kwenye ubongo hutegemea kupata virutubisho na oksijeni kutoka kwenye damu. Kukosa damu hata kwa dakika moja, huathiri kwa kiasi kikubwa uafanyaji kazi huu. Seli hizi zinaweza kufa kabisa kama zikikosa damu kwa dakika 5, na huwa haziwezi kutengeneza seli mpya.

Kwa hiyo pale inapotokea mshipa wa
damu wa sehemu fulani ya ubongo umeziba au kupasuka, damu hushindwa
kufika kwenye sehemu hiyo na hivyo seli zake zitashindwa kufanya kazi
vizuri. Hali hii ikiendelea zaidi, seli hizo zitakufa kabisa. Kila
sehemu ya ubongo huratibu kazi maalumu mwilini, mfano kuongea. Seli
zinazoratibu kazi fulani zinapokufa, kazi hizo hushindwa kufanyika tena
na hivyo dalili za kiharusi hujitokeza ikitegemea na sehemu ya ubongo
iliyoathiirika.
KUNA AINA MBILI YA KIHARUSI:
Kiharusi
kutokana na mishipa ya damu kuziba kwenye ubongo (ischemic
stroke)kiharusi kutokana na mishipa ya damu kupasuka kwenye ubongo
(hemorrhagic stroke)
Mishipa ya damu kuziba kwenye ubongo (ischemic stroke) ni aina ya kiharusi kinachojitokeza zaidi kwa kiasi cha silimia 80, asilimia nyingine hutokana na mishipa ya damu kupasuka.
Mishipa ya damu kuziba kwenye ubongo (ischemic stroke) ni aina ya kiharusi kinachojitokeza zaidi kwa kiasi cha silimia 80, asilimia nyingine hutokana na mishipa ya damu kupasuka.
DALILI ZA KIHARUSI
Ugonjwa huu unaweza kujitokeza haraka na ghafla bila kutarajia. Na dalili hizi zinaweza kutokea kwenye sehemu yoyote ya mwili. Unapopata kiharusi unaweza kupata dalili zifuatazo:
Ugonjwa huu unaweza kujitokeza haraka na ghafla bila kutarajia. Na dalili hizi zinaweza kutokea kwenye sehemu yoyote ya mwili. Unapopata kiharusi unaweza kupata dalili zifuatazo:
Kushindwa
kuongea au kuelewa. Unaweza kupatwa na hali ya kuchanganyikiwa,
kushindwa kuongea ua kuelewa ghafla.Kukosa nguvu au ganzi upande mmoja
wa mwili. Ghafla tu unaweza kupatwa na hali ya kukosa nguvu, ganzi
kwenye uso, mkono au mguu, hasa upande mmoja wa mwili. Mdomo kuelekea
upande mmoja unapocheka, kushindwa kunyanyua mkono upande
mmoja.Kushindwa kuona vizuri. Hali ya kushindwa kuona vizuri inaweza
kujitokeza ghafla. Inaweza kuwa kwa macho yote au jicho moja
tu.Kushindwa kutembea. Ghafla tu unaweza kushindwa kutembea kutokana na
kupata kizunguzungu kikali, kukosa uwiano kwa ghafla.Maumivu makali ya
kichwa ghafla.Dalili nyingine ambazo unaweza kupata ni kupoteza fahamu,
degedege (convulsions), kushindwa kula, kushindwa kuzuia choo.
Kiharusi ni ugonjwa unaohitaji matibabu haraka sana. Kadri mgonjwa anapozidi kuchelewa kupata mtibabu ndivyo seli za ubongo zinavyozidi kufa. Kufa kwa seli hizi kutasababisha ulemavu kwa mgonjwa.
Kiharusi ni ugonjwa unaohitaji matibabu haraka sana. Kadri mgonjwa anapozidi kuchelewa kupata mtibabu ndivyo seli za ubongo zinavyozidi kufa. Kufa kwa seli hizi kutasababisha ulemavu kwa mgonjwa.
SABABU HATARISHI ZA KIHARUSI KUTOKEA
Vitu au tabia zifuatazo huongeza hatari ya kiharusi kutokea kwako:
Vitu au tabia zifuatazo huongeza hatari ya kiharusi kutokea kwako:
Shinikizo
la Damu La KupandaUvutaji sigaraMagonjwa ya moyoMagonjwa kama
KisukariKiwangi kikubwa cha lehemu kwenye damuKutofanya mazoeziUzito
mkubwaUnywaji wa pombe kiholela
VIPIMO
Unapopata tatizo hili unaweza kufanyiwa vipimo vifuatavyo ili kujua aina ya kiharusi ili upate matibabau sahihi.
Unapopata tatizo hili unaweza kufanyiwa vipimo vifuatavyo ili kujua aina ya kiharusi ili upate matibabau sahihi.
Vipimo Vya Damu:
Complete Blood CountClotting factorsKipimo cha CT Scan ya UbongoKipimo cha MRI ya Ubongo
KUJIKINGA NA KIHARUSI
Kujikinga usipate kiharusi ni kitu muhimu sana, kwani hauwezi kujua kikitokea kitakuathiri namna gani. Kuna tabia hatarishi nyingi ambazo unaweza kuziondoa ka kufanya mabadiliko fulani katika maisha yako kama tutakavyoona hapo chini.

Acha kuvuta
sigaraShinikizo la damu la kupanda (hypertension). Fanya mazoezi, kula
mlo kamili, dhibiti uzito,punguza chumvi na tumia dawa kudhibiti
presha.Kisukari.Magonjwa ya moyo.Fanya Mazoezi.Dhibiti Uzito Wako.
Ukijenga utamaduni wa kutembelea ukurasa huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mali, maarifa na afya. Kazi kwako!
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT