Karibu sana mwanamafanikio mwenzangu katika ukurasa wetu huu uliojaa shule isiyolipiwa ada! Jambo la maana zaidi ni kumshukuru mwenyezi Mungu kutupa nafasi ya kuiona leo na zaidi kupata kuona link iliyokuleta hapa ili upate elimu hii ambayo huenda pengine ungelazimika kuilipia au kutoipata kabisa! Leo nakupa namna ambavyo unaweza kuwa mbunifu katika mazingira unayoishi. Karibu tuwe pamoja.
Mambo haya chini ukiyafanyia kazi yataweza kukufanya kubadilika na kuweza kuwa mbunifu katika mazingira unayoishi.
1. WAZA TOFAUTI FANYA TOFAUTI (Think different,act differently)
Usiishi na mawazo yale yale na usikubaliane na utamaduni uliopo kila siku wa kufanya mambo yale yale yale .Njoo na kitu kipya .
Mtu mmoja alijiuliza kwa nini alikuwa hauzi bidhaa zake wakati huo jirani yake anayeuza bidhaa zile zile alikuwa akiuza sana .Kama ilivyo kawaida kwa watu wenye mitazamo hasi ndugu huyu alidhani mwenzake anatumia uchawi kutoka kwa wagaganga kumbe ni ubunifu tu .Wakati yeye alikuwa alikuwa hachukui mawasiliano ya wateja mwenzake kila mteja anayekuja alikuwa anachukua mawasiliano yake na kila bidhaa iliyokuwa iko dukani alikuwa akiwatumia wateja wake meseji kuwaeleza kile alichonacho.Wakati mwingine baadhi ya wateja aliwapigia simu na kuwajulia hali huku kila siku akiwatumia sms za kuwatakia kila la kheri .Wateja hawa walianza kupenda jinsi huyu ndugu alikuwa anawajali na hawakuacha kwenda kununua vitu kwake pale walipotaka kununua bidhaa na akawa anauza sana huku jirani yake akidhani ni Uchawi_
(Wewe unafanya nini cha tofauti kwenye biashara yako???? unajua umekosa wateja wangapi kwa kukosa ubunifu???
2. MWANYA(Find The Gap)
Kama unataka kuwa mbunifu eneo lolote , unapaswa kutafuta wapi kuna mwanya ili uweze kutumia mwanya huo kwa tija .Bado kuna mianya mingi sana ambayo iko wazi ,ina msubiri mtu mbunifu aitumie .
Wakati mwingine mimi nilikuwa nawaza namna ambavyo wauza genge wangeweza kuwa wabunifu na kuanza kufanya huduma ya kusambaza viungo majumbani bila kusubiri wateja kuwafuata .Hii ni fursa ambayo hata wewe waweza kuitumia eneo ulipo .Kama muuza genge angeamua kununua mkokoteni na akaanza kusambaza viungo majumbani huku kwenye banda lake akimwachia mtu naamini mtu huyu angetengeneza pesa nyingi sana maana kwa asili watanzania wengi ni wavivu na hivyo ukiwafuata maana yake umewasaidia (Hawataki kujichosha )
3. TAFUTA MAARIFA(SEEK KNOWLEDGE)
Mara nyingi ukiona siyo mbunifu eneo ulipo jua kuwa huna maarifa na hicho kitu unachokifanya na hivyo una kila sababu ya kutafuta maarifa juu ya hicho kitu .Ukipata maarifa nakuhakikishia lazima utafanya kwa utofautii kabisa .Acha uvivu kabisa wa kutafuta maarifa kama unataka kufanya kwa tofauti .Tumia muda mwingi kujifunza .Maarifa ni uwekezaji mzuri sana na ni bahati mbaya kuwa watu wengi hawalijui hili na wamebaki kama walivyo na miaka yao si rafiki lakini habari njema ni kwamba muda ni sasa hujachelewa anza kutafuta maarifa. Bila maarifa utajua jirani yako yuko kwenye chama cha FREEMANSON kumbe amekuzidi maarifa.

Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mali, maarifa na afya. Kazi kwako!
*JYB 0753836463*
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT