Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam huku akionya kuwa kiongozi yeyote ambaye hayupo tayari kutekeleza agizo hilo aachie ngazi.
Rais amelaumu tabia ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuwafukuza Wamachinga bila utaratibu wowote wa wapi wanawapeleka na wakati mwingine wanapelekwa maeneo ya mbali ambayo hayafai hata kwa kufanya biashara,ambapo amesisitiza kwamba jambo hilo siyo sawa.
Hata hivyo Rais Magufuli amesema maagizo yake hayana maana kuwa Wamachinga na Wachimbaji wadogo waendeshe shughuli zao kwa kuvunja sheria bali wazingatie sheria na Mamlaka zisiwanyanyase watu wanyonge.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT