KIINUA MGONGO NA BIASHARA | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Alhamisi, 10 Novemba 2016

KIINUA MGONGO NA BIASHARA

Habari mwanafaniko mwenzangu. Nashukuru kwa kiu yako ya kutaka kujua mbinu za kukufanya ufanikiwe kimaisha an kuweza kuja hapa jamvini kwangu.Image result for kiinua mgongo
 
Leo nimeona niongee na wastaafu wote na wastaafu watarajiwa. Nawapongeza kwa utumishi uliotuka katika taifa letu la Tanzania. Mmelitumikia taifa hili kwa kipindi kirefu sana na mnastahili pongezi nyingi nyingi. Wazee wangu baada ya utumishi huu kifuta jasho hutolewa kwa ajili yenu. Hapa ndipo sintofahamu huibuka kwani miezi michache baada ya kupokea kiinua mgongotu maisha hubadilika, mzee anahama nyumbani na kuitelekeza familia yake na kutokomea kusikojulikana na wengine huamua kujiingiza katika BIASHARA ili mradi tu kuionesha jamii inayokuzunguka kuwa wewe ni tajiri. Kundi lingine la wastaafu huangukia kwenye baa za pombe na kufunga milango na kutoa ofa za vinywaji. Hii kitu huniumiza kichwa sana na kujiuliza kwa nini inakuwa hivi?
Lakini tuachane na hilo leo nitatembea njia moja na WASTAAFU wenye Ndoto ya kuanzisha miradi au biashara. Kabla ya kuanza biashara au mradi kitu cha kwanza jiulize umewahi kufanya biashara au mradi huo? Kama jibu ni ndiyo basi anza biashara au mradi huo kwa kuanza na mtaji kidogo kwanza ili kuona kama biashara yako ni rafiki katika eneo hilo, ukiona inatoka basi anza kuongeza mtaji kidogo kidogo hadi kufikia pale ulipo tarajia. Pia ningekushauri ufanye biashara ya Ndoto yako nikimaanisha fanya biashara ambayo muda mrefu ulikuwa ukiifikia kuifanya. Japo tunashauri sana kabla ya kuanza biashara fanya utafiti kwanza ni biashara ipi inafaa katika eneo hilo.
Kamwe usiitumie hela ya kiinua mgongo kujengea nyumba au kununua magari yasiyo na mpango. Bila shaka tumetembea pamoja nami katika safari hii fupi lakini ikilenga kujenga. Kwa maoni na ushauri juu ya safari hii, nicheki kupitia mawasiliano yangu hapa chini...
. . . . . . . . . . . . 0764857776 au 0625728742 au kwa email :edwinsoloma73@gmail.com 

Usiache kutembelea ukurasa huu kila siku kupata vitu vipya vya kukujenga. Karibu sana
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT