Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa
amesema anakiandaa kikosi chake vizuri ili kuhakikisha kinafanya vizuri
katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe utakaopigwa Novemba 13 mwaka
huu.
Akizungumza na Hot Mix Michezo, Mkwasa amesema, kikosi cha Zimbabwe kitakuwa kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo utakaokuwa na ushindani na kwa upande wake pia ameandaa kikosi chake na amekwishapokea wachezaji aliowaita katika timu hiyo huku mchezaji wa Azam FC David Mwantika akishindwa kuingia kambini kutokana na kuwa majeruhi.
Mkwasa amesema, wachezaji wa kimataifa pia wameshawasili kambini ambao ni Elias Maguli, Mbwana Samatta pamoja na Thomas Ulimwengu ambaye ni mchezaji huru.
Mkwasa amesema, mara baada ya kupata taarifa kuwa Mwantika ni majeruhi alimuita Aggrey Morris ambaye naye pia aliambiwa ni majeruhi lakini anaamini kwa wachezaji alionao atapata mtu wa kucheza nafasi ambazo zitakuwa na majeruhi.
Kikosi cha Stars kinatarajiwa kuondoka kesho jioni kuelekea nchini Zimbabwe ambapo kabla ya safari kesho asubuhi kikosi hicho chenye wachezaji 23 mpaka sasa mara baada ya Mwantika kuwa majeruhi kitafanya mazoezi ambapo kocha atachagua wachezaji 20 anaotakiwa kuondoka nao kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa mwishoni mwa wiki hii.
SOMA: Kauli ya Mkhitaryan kuhusu kupewa nafasi ndogo na Mourinho

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT