Zabibu hutumika kutengeneza divai, lakini pia huweza kuliwa kama tunda. Tunda hili huweza kuwa katika rangi mbalimbali na katika kichana chenye zabibu 6 hadi 300.
Matunda haya inaelezwa kwamba
yalianza kulimwa huko nchini Uturuki, lakini kwa hapa nchini kwetu
Tanzania yanapatikana sana mkoani Dodoma.
Matunda
haya huwa na rangi ya nyekundu iliyoiva, nyeusi, bluu ya kukoza ,
njano, kijani na hata pinki, licha ya kwamba hapa kwetu Tanzania wengi
tumezoea zabibu za rangi nyeusi
Kwa mujibu wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani (FAO)
linaeleza kuwa asilimia 71 ya zabibu yote duniani hutumika kutengenezea
mvinyo na asilimia 27 huliwa kama matunda ya kawaida, huku asilimia 2
ikifanywa kukaushwa.
Zabibu husaidia kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo.
Aidha,
inaeleza kwamba zabibu pia husaidia damu kuwa nyepesi na kuzuia
isigande ndani ya mishipa ya damu, hivyo kutokana na sababu hii
hupunguza hatari ya kukumbwa na kiharusi (stroke). Kunywa juisi ya
zabibu nyekundu (red grapes) kuzuia damu kuganda ili kupunguza hatari ya
magonjwa ya moyo.
Utafiti uliofanyika mwaka
2005 kwa watu 1000 wenye matatizo ya magonjwa ya moyo ulibaini kwamba
asilimia 50 ya watu hao matatizo yao ya shambulio la moyo (heart attack)
au kurudiwa na kiharusi yalipungua kwa kunywa divai nyekundu (red wine)
kiasi cha glasi moja kila siku wakati wa kula chakula.
Kwamba
zabibu pia inasaidia kuzuia na kutibu tatizo la upungufu wa damu na pia
kwa wale wanaotumia mara kwa mara tunda hili huwasaidia kuepukana na
ugonjwa wa bawasiri (Hemorrhoids).
Kadhalika
matunda hayo husaidia katika tiba na kinga ya magonjwa ya ini kutokana
na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na
kuzalisha nyongo kwa wingi.
Zabibu pia husaidia kuimarisha afya ya figo na kuifanya kuwa na uwezo zaidi katika katika kuondosha sumu ndani ya damu .
Mbali na faida hizo, pia zabibu kutokana na kuwa na sukari ya asili aina ya fructose na glucose hivyo huweza kumsaidia mtu katika kupunguza uchovu wa mwili na kutibu maumivu yasiyokuwa na sababu za moja kwa moja.
Sambamba
na hayo, watalaam wa afya hueleza kuwa juisi ya zabibu (divai) husaidia
tumbo na utumbo kufanya kazi vizuri na kuzuia ukavu wa haja kubwa ,
lakini pia divai huimarisha afya ya mishipa ya damu katika mfumo wa
kumeng;enya, kusaga na kusharabu chakula na viini lishe.
Divai
pia husaidia bacteria rafiki kwa binadamu wanaoishi ndani ya tumbo
(normal flora) kukua vizuri na kusababisha umeng’enyaji wa chakula ndani
ya tumbo kuwa rahisi.
Kutokana
na madini yaliyomo ndani ya zabibu huifanya divai kuwa dawa nzuri
inayopunguza maumivu ya tumbo yanayotokana na kujiminya kwa misuli ya
kuta za matumbo (antispasmodic effect).
Kwa
wale wanaotaka kupunguza miili yao (slimming) na kuimarisha afya ya
miili yao wanashauriwa kunywa juisi ya zabibu siku moja kila juma bila
kula chakula kingine chochote siku hiyo. Na siku zingine za wiki
wanapaswa kula mlo kamili (balanced diet).
Wataalam
hushauri kwamba ni vizuri ukatumia kila siku japo punje za zabibu
zisizopunguwa tano kwa ajili ya kulinda afya ya mfumo wa damu na nyama
za moyo.
Kwa moyo wangu
wa upendo wa kushea na wewe habari njema inayohusu afya ya mwili na
akili yako nakuomba pia kwa upendo huo huo usiache kutembela ukurasa huu
kila siku kupata jambo jipya kuhusu afya yako. AFYA NDIO MTAJI WAKO WA
KWANZA
Usisahau kushea ukurasa huu uokoe wengi. Barikiwa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT