Leo mapema Bungeni, Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekubaliana kwa kauli moja kuwa posho za kila mbunge kwa siku ya leo zipelekwe kwa wazazi wa wanafunzi waliofariki kwa ajali ya basi la Shule ya awali na Msingi ya Lucky Vincent. Kiasi hicho pamoja na mchango wa speaker, umefikia kiasi cha Milioni 200.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Hata hivyo licha ya wabunge kutoa rambi rambi hizo Serikali wiki iliyopita ilitangaza kugharamia gharama zote za mazishi ya vifo hivyo.
By Godfrey Mgallah
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT