Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ambao hutumiwa na
serikali ya Marekani kutoa misaada kwa nchi za nje, limesitisha ufadhili
wake kwa miradi ya afya nchini Kenya.
Taarifa kutoka shirika hilo limesema kuwa kusitishwa kwa misaada yote
yanayohusu masuala ya wizara ya afya na ni kutokana na Kenya kutotimiza
masharti ambayo waliwapatia.
Hatua hiyo ya Marekani kusitisha misaada kunatarajiwa kuathiri shughuli
mbali mbali za kiserikali ikiwemo ya mapambano dhidi ya malaria, kifua
kikuu na Ukimwi pamoja na miradi ya uzazi wa mpango, huduma za afya kwa
waja wazito na watoto.
Mnamo mwaka jana Desemba madaktari wakenye waligoma kwa siku 100, pia
mkaguzi mkuu wa hesabu nchini humo alisema jumla ya dola milioni 50
hazikutumika katika wizara ya afya kama ilivyo tarajiwa.
Hata hivyo maafisa katika wizara ya afya pamoja na baadhi ya viongozi
nchini humo walidaiwa kuhusika katika ufujaji wa pesa hizo, lakini
Wizara ya nchi hiyo ilijitetea kwa kukanusha habari hizo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT