Mbunge wa jimbo la Mikumi Mh. Joseph Haule amefunguka na kuitaka
serikali kuwekeza fedha za kutosha katika Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo ili wizara hiyo iweze kuwekeza katika sanaa na kuacha
kuwatumia wasanii kama makarai ya kujengea.
Prof Jay alisema hayo Bungeni wakati akichangia makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari kwa mwaka 2017/ 2018
"Wasanii wa Tanzania wamekuwa katika mazingira magumu sana na wamekuwa
katika umasikini mkubwa licha ya mara nyingi kutumiwa katika kampeni
mbambali na hata katika chaguzi zilizopita mmeona jinsi wasanii
walivyokuwa wakitumika, mmewatumia kama makarai na baada ya hapo
mmeyaweka uvunguni, tunajua makarai huwa yanatumika kwenye kujenga
maghorofa na vitu vingine lakini nyumba ikikamilika yanawekwa uvunguni
hayatakiwa kuonekana hata kwa wageni" alisema Prof Jay
Mbali na hilo Prof Jay amesema wasanii wengi wa Tanzania wanakuwa
masikini sana sababu wakishatumika huwa hawathaminiwa tena na kuachwa
mpaka wakati mwingine wa uchaguzi au kampeni
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT