Siku chache baada ya wabunge kueleza kutoridhishwa na Serikali kuhamia
kwenye majengo ya Chuo Kikuu Dodoma (Udom), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii nayo imepinga hatua hiyo.
Kamati hiyo pia imeshauri Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), kuachana na
utaratibu wa kupangia wanafunzi vyuo na ijikite kusimamia ubora wa elimu
inayotolewa na vyuo vikuu nchini.
Mapendekezo hayo yalitolewa bungeni mjini Dodoma jana na Mwenyekiti wa
kamati hiyo, Peter Serukamba alipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa
shughuli za kamati hiyo kwa mwaka 2016.
Serukamba ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema kamati hiyo ya
Bunge inaunga mkono Serikali kuhamia Dodoma, lakini utaratibu wa wizara
kuhamishia ofisi zao Udom siyo sawa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT