Mlinzi jela miaka miwili kwa kuua bila kukusudia | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumatatu, 6 Februari 2017

Mlinzi jela miaka miwili kwa kuua bila kukusudia

Shinyanga. Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, imemhukumu kifungo cha miaka miwili jela Juma Msanja (35) baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia.

Jaji Victoria Makani, akitoa hukumu alisema ameridhika na ushahidi uliowasilishwa mahakamani dhidi ya mshtakiwa aliyekuwa mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya Zeneth inayolinda mgodi wa almasi wa Williamson, ambaye pia alikiri kutenda kosa hilo.

Awali, Wakili wa Serikali, Pendo Makondo alidai  Septemba 24, 2014 akiwa na bunduki aina ya Shotgun, mshtakiwa alifyatua risasi nne hewani na alimpiga Vene Edward (28), mkazi wa Maganzo wilayani Kishapu na kusababisha kifo chake.

Alidai siku ya tukio mshtakiwa akiwa na walinzi wenzake mgodini eneo la Mwadui wilayani Kishapu, waliona kundi la watu lililovamia mgodi na kuchimba mchanga unaodaiwa kuwa na madini ya almasi.

Makondo alidai mshtakiwa na wenzake walikwenda kuwafukuza watu hao ambao waliwashambulia kwa silaha za jadi ndipo alipofyatua risasi hewani ambazo zilimpata Edward na kusababisha kifo chake.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT