Sakata la wasanii 12 wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi limezidi kukua baada ya watu wengine 100 kukamatwa.
Kati ya watu 112 ambao wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za
kujihusisha na utumiaji au biashara ya dawa hizo, 12 kati yao
wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo baada ya kazi hiyo kushindikana
jana.
Miongoni mwa watuhumiwa wanaotarajiwa kupandishwa kizimba cha Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, ni mwigizaji maarufu wa filamu Wema Sepetu na
msanii mwenzake Omary Micheri ambao polisi wamedai walikutwa na
vielelezo vya dawa za kulevya na bangi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Siro
alisema watawafungulia watuhumiwa maombi ya kuwaweka chini ya uangalizi
wa mahakama na polisi kwa muda wa miaka miwili na watakuwa wakiripoti
kituo cha polisi mara mbili kwa mwezi.
Siro alisema kati ya watuhumiwa 12 waliokamatwa kwanza, 10 walikiri
kutumia dawa hizo na kuwataja wauzaji lakini wawili walikutwa na
vielelezo nyumbani kwao.
Alisema Wema, ambaye aliwahi kushinda taji la mrembo wa Tanzania (Miss
Tanzania), alipekuliwa nyumbani kwake na kukutwa na misokoto ya bangi na
makaratasi yake, wakati Micheri alikutwa na kete tatu za dawa za
kulevya ambazo hazijajulikana za aina gani hadi zitakapofanyiwa
uchunguzi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT