Chama cha Wananchi (CUF) kimesema hakitafanya mazungumzo kusaka suluhu
na mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na msajili wa
vyama vya siasa na kwamba, kipo tayari kwa lolote hata kama kitafutiwa
usajili.
Pia, chama hicho kimesema hakijuti kumkaribisha na kumuunga mkono Edward
Lowassa, ambaye aliteuliwa kugombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya
Chadema na kuwakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Maelezo hayo yalitolewa juzi na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa
CUF, Mbarala Maharagande kujibu madai yaliyotolewa na Profesa Lipumba
alipohojiwa katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na kituo cha
televisheni cha Azam.
Katika mahojiano hayo, Profesa Lipumba alidai kuwa mgogoro uliopo ndani
ya chama hicho kwa sasa hautamalizwa na mahakama pekee bali viongozi wa
pande mbili na kuzungumza, lakini Maharagande amesema haiwezekani kwa
vile Lipumba alishakwisha kukivuruga na hafai tena kuendelea kuwa
kiongozi.
“Lipumba anasema tukae tulimalize suala hili kwa kuongea sisi wenyewe.
Jambo hilo haliwezekani kwa kuwa kama kupandikiza chuki, uhasama,
uharibifu wa chama miongoni mwa wanachama na viongozi ameshafanya na
kufanikiwa hilo kwa baadhi ya wanachama na viongozi wake na kuharibu
taswira ya chama kwa jamii,” alisema Maharagande.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT