NHC yatakiwa kuwalenga watu wa kipato cha chini | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumatatu, 6 Februari 2017

NHC yatakiwa kuwalenga watu wa kipato cha chini


Dodoma. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeagizwa kujenga nyumba za gharama nafuu mkoani Dodoma ili zinunuliwe na watu wa kipato cha chini.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alitoa agizo hilo juzi alipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa eneo la Iyumbu, nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Mkurugenzi wa NHC, Nehemiah Mchechu alisema kuna mkakati mwingine wa kujenga nyumba za gharama tofauti ikiwamo zitakazowalenga watu wa kipato cha chini.

Mchechu alisema watatumia eka 200 walizobakiza ili kuharakisha ujenzi ambao unakwenda sambamba na miundombinu yote.

Alisema utekelezaji wa mradi huo unafanyika sanjari na hatua ya Serikali kuhamia Dodoma na kwamba, lengo ni kuhakikisha wanatatua tatizo la makazi kwa watumishi watakaohamia.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT