WAZIRI
Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali inayoongozwa na Rais John
Magufuli inasimamia nidhamu ya kazi na heshima kwa wananchi, hivyo
kutaka kila mmoja atimize wajibu wake.
Aidha,
imeonya kuwa fedha za miradi ya serikali ni za moto hivyo ziachwe
sifanye shughuli zilizokusudiwa, kwani zikichezewa lazima zitaunguza mtu
au watu.
Aliyasema
hayo jana jioni alipozungumza na wananchi wa Jiji la Arusha
waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Alisema
serikali imeamua kupanua wigo wa kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika
na serikali yake kwa kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali.
Alisema
serikali inaendelea kuwahudumia wananchi na kuwataka wakurugenzi, wakuu
wa mikoa na wilaya kusimamia maendeleo ya wananchi huku akimpongeza
Gambo kwa kufanya kazi za kuwahudumia wananchi.
Pia
amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kukutana na watoa
huduma wa magari ya Noah yanayosafirisha abiria maeneo mbalimbali ili
kutatua changamoto zao ikiwemo usumbufu wa usafirishaji wanaopata.
Alimpongeza
kwa kuwezesha kuibua ajira kwa vijana na kumwagiza Mkurugenzi wa Jiji
la Arusha, Athumani Kihamia kuhakikisha vijana wanapewa maeneo ya
kufanya biashara.
Waziri
Mkuu pia alitoa rai kwa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuangalia jinsi
ya kukusanya ushuru kwa kinamama wafanyabiashara wanaotembeza bidhaa zao
kwenye mabeseni jijimo humo ili waweze kujikwamua.
Katika
mkutano huo, Waziri Mkuu alikabidhi pikipiki zaidi ya 200 kwa waendesha
bodaboda ili waweze kujikwamua kiuchumi. Awali, kabla ya Waziri Mkuu
kuzungumza na wananchi, Gambo alimpongeza Meya wa Jiji la Arusha, Calist
Lazaro (Chadema) kwa kuungana na falsafa ya Hapa Kazi Tu.
Alisema alipoingia mkoani hapo alikuta Diwani analipwa Sh 150,000 kila mwezi na vocha ya simu Sh 100,000.
“Tuliona
hili hapana na tulikata fedha hizo za madiwani tukalipa madeni ya
walimu. Kuhusu maeneo ya wazi, tumempa orodha Rais ya hayo maeneo na
tunasubiri maamuzi yake kwa ajili ya miradi ya maendeleo,” alisema.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT