Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe
Mama Janeth Magufuli wametoa mchango wa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya
kusaidia matibabu ya mtoto Haidari Bonge mwenye umri wa miaka 7
anayesumbuliwa na tatizo la kuota nyama kichwani, mdomoni na machoni.
Mtoto
huyo anayeishi Mbagala Kuu Jijini Dar es Salaam alianza kuotwa na nyama
miezi mitatu baada ya kuzaliwa na amekuwa akifanyiwa upasuaji wa
kuondoa nyama hizo mara kwa mara.
Rais
Magufuli ametoa ahadi hiyo mara baada ya kutazama kipengele cha
Hadubini “Habari kwa Kina” kilichorushwa hewani katika taarifa ya habari
saa 2 usiku na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jana tarehe 03
Desemba, 2016.
“Mimi
na Mke wangu tumeguswa na tatizo linalomkabili Mtoto Hidari Bonge na
tumeamua kuchangia Shilingi Milioni 5 kutoka kwenye mshahara kwa ajili
ya kuchangia matibabu yake.
“Pia
tunatoa pole kwake na kwa familia yake ambayo imekuwa ikifanya juhudi
kubwa za kuhakikisha anapatiwa matibabu kwa kipindi kirefu cha miaka 7
sasa” amesema Rais Magufuli.
Mchango huo utakabidhiwa leo tarehe 04 Desemba, 2016.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT