SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limetimiza agizo la Rais John Magufuli la kukipatia umeme kiwanda cha kusindika matunda cha Azam Fruits Processing Plant, mali ya mfanyabishara, Said Salim Bakhresa kabla ya muda wa miezi miwili waliyopewa kukamilisha kazi hiyo.
Rais
Magufuli alitoa agizo hilo Oktoba 6, mwaka huu alipokuwa anazindua
kiwanda hicho kilichopo Mwandege, Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani
kufuatia kilio kilichotolewa na uongozi wa kiwanda hicho kuiomba
serikali iingilie kati ili kupata umeme wa uhakika kwa ajili ya
uzalishaji bidhaa kiwandani hapo.
“Tayari
tumetimiza agizo la Rais la kukipatia umeme kiwanda cha Bakhresa,
Mkuranga Novemba 30, mwaka huu kwa kufikisha umeme kiwandani hapo,”
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba alitoa maelezo hayo
jana jijini Dar es Salaam.
Mramba
alikuwa anatoa majumuisho kwa wahariri wa vyombo vya habari baada ya
ziara ya kutembelea miradi ya ukarabati wa miundombinu ya usambazaji
umeme jijini Dar es Salaam.
Alifafanua
umeme umefikishwa kiwandani hapo na kilichobaki ni upande wa kiwanda
chenyewe ambao unasubiri baadhi ya vifaa kutoka nje ili waweze kuingiza
umeme ndani ya kiwanda.
Alisema
Tanesco inajenga njia tatu za umeme kuelekea Mkuranga na mbili kati
hizo ni kwa ajili ya viwanda vipya wilayani humo na moja kwa ajili ya
matumizi ya nyumbani.
Katika
juhudi za kuboresha miundombinu ya Tanesco ili kukidhi adhma ya
serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa viwanda, shirika lake
linatekeleza miradi ya ukarabati wa miundo mbinu ya umeme kwa nchi nzima
itakayogharimu Sh zaidi ya trilioni 5.4.
Alifafanua
miradi hiyo ni pamoja na uzalishaji, usafirishaji na vituo vya
kusambazia umeme ambavyo mifumo ya zamani ya analogia inabadilishwa na
kuwekwa mifumo mipya ya ya kisasa ya dijitali yenye ufanisi mzuri zaidi.
Vituo
vya usambazaji umeme vya Dar es Salaam vilivyotembelewa vikiwa bado
vinaendelea na ukarabati wa mifumo ya zamani na kuweka ya kisasa ni
pamoja na Muhimbili, City Center, Sokoine na Kituo cha Ilala.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT