Waomba wanaofeli la 7 waende sekondari | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Alhamisi, 1 Desemba 2016

Waomba wanaofeli la 7 waende sekondari

WADAU wa elimu mkoani Shinyanga wameiomba Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, iruhusu wanafunzi wa darasa la saba waliofeli kujiunga na kidato cha kwanza, warudie mitihani kama wanavyofanya wa kidato cha nne na sita.

Wamesema hatua hiyo ichukuliwe kama njia ya kumaliza tatizo la watu wasiokuwa na elimu bora ya msingi nchini.

Wadau hao waliyabainisha hayo juzi wakati Mkoa wa Shinyanga ulipochambua na kutoa matokeo ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidacho cha kwanza mwakani.

Amesema wanafunzi 16,907 wamechaguliwa, kati yao wavulana ni 8,387 wasichana 8,520 kati ya wanafunzi 25,413 waliofanya mtihani.

Wanafunzi 8,506 walifeli.

"Wizara ya elimu iangalie utaratibu wa kuruhusu wanafunzi wa darasa la saba wanaoshindwa kupata alama za kuendelea na kidato cha kwanza, warudie mitihani yao ili kutoa fursa kwa wanafunzi hao wafaidi matunda ya elimu bure na kumaliza taifa la wajinga," amesema diwani wa Kambarage, Hassan Mwendapole.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela alisema ufaulu wa wanafunzi mkoani humo umeongezeka.

Amesema mwaka 2015 mkoa ulikuwa nafasi ya 13, mwaka 2016 nafasi ya 15 kati ya mikoa 26 sambamba na shule mbili za Kwema na Roknehill kushika nafasi ya kwanza na pili kitaifa.

Msovela alisema kati ya wanafunzi hao waliochanguliwa kujiunga kidato cha kwanza, 29 wamechaguliwa vipaji maalumu, wa bweni 24, wengine 32 vyuo vya ufundi.

Ofisa wa Eimu wa Mkoa wa Shinyanga, Mohamed Kahundi, alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi mkoani humo kujenga tabia ya kuwawahisha watoto kupata elimu ya awali.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT