MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo
ameinusuru timu yake, KRC Genk kulala nyumbani mbele ya Standard Liege
katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
Samatta ameifungia bao la kusawazisha Genk katika sare ya 2-2 na Liege Uwanja wa Laminus Arena mjini Genk.
Na mchezaji huyo wa zamani wa Simba alifunga bao hilo dakika ya 77 akimalizia pasi ya beki Jere Uronen kutoka Finland.
Katika mchezo huo, ambao mshambuliaji wa Uganda, Faruk Miya alikuwa
kwenye benchi la Liege muda wote, Genk walikuwa wa kwanza kupata bao
lililofungwa na beki Mgambia Omar Colley dakika ya tatu, akimalizia pasi
ya mshambuliaji Mjamaica, Leon Bailey.
Samatta (kulia) ameifungia bao la kusawazisha Genk katika sare ya 2-2 na Liege Uwanja wa Laminus Arena mjini Genk
Standard Liege ikatoka nyuma na kuongoza kwa 2-1 kwa mabao ya
washambuliaji Mreno Orlando Sa dakika ya 15 na Mualgeria Ishak Belfodil
dakika ya 25.
Huo unakuwa mchezo wa 35 jumla kwa Samatta kucheza Genk tangu awasili
Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC),18 msimu uliopita na 17 msimu huu.
Kati ya hizo, ni mechi 17 tu alianza, 10 msimu uliopita na saba msimu
huu, 18 alitokea benchi, nane msimu uliopita na 10 msimu huu, wakati
nane hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na mbili msimu
huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao tisa, manne msimu huu na matano
msimu uliopita.
Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Bizot, Walsh/Uronen dk76, Colley, Dewaest,
Castagne, Ndidi, Pozuelo, Samatta, Trossard/Buffalo dk72, Bailey na
Karelis.
Standard Liege : Hubert, Goreux, Elderson, Raman/Mbenza dk39,
Edmilson/Fiore dk81, Trebel, Kosanovic, Laifis, Cisse, Sa/Dompe dk63 na
Belfodil.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT