Arsenal wamaliza vinara kundi lao UEFA | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumanne, 6 Desemba 2016

Arsenal wamaliza vinara kundi lao UEFA

Lucas Perez alikuwa amefungia Arsenal magoli mawili pekee awali kabla ya 'hat-trick' hiyo Basel
Arsenal wamefanikiwa kuwaliza kileleni katika Kundi A Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya FC Basel ya Uswizi.

Ufanisi huo ulitokana na mabao matatu aliyoyafunga kiungo Lucas Perez na kuwawezesha kushinda 4-1.

Wapinzani wao Paris St-Germain, ambao kabla ya mechi za Jumanne walikuwa wanaongoza kundi, walishuka na kumaliza nambari mbili baada ya kutoka sare na Ludogorets Razgrad wa Bulgaria mjini Paris.

PSG wangefanikiwa kumaliza vinara iwapo wangeshinda mechi hiyo, lakini hilo halikuwa.
Borussia Dortmund na Legia Warsaw wavunja rekodi

Perez alifungua Arsenal mabao matatu nalo la nne likatoka kwa Alex Iwobi kabla ya Seydou Doumbia kufungia Basel bao la kufutia machozi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Arsenal kumaliza kileleni kundi lao tangu msimu wa 2011-12.
Hata hivyo, vijana hao wa Arsene Wenger hawakufanikiwa kusonga zaidi ya hatua ya 16 bora mwaka huo.

Wamekuwa wakiondolewa kwenye michuano hiyo hatua hiyo ya muondoano kila msimu kwa misimu sita iliyopita.

Kando na kufanikiwa kumaliza kileleni Gunners, pia wamefanikiwa kumaliza michuano ya hatua ya makundi bila kushindwa kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2005-06, msimu ambao walifika fainali.

Gunners' good fortune?

Drooo ya hatua ya makundi itafanyika Jumatatu na Arsenal wamefanikiwa kuwakwepa Barcelona na Monaco, waliowaondoa kwenye michuano misimu miwili iliyopita. Aidha, wamewahepa pia Atletico Madrid na Napoli.

Hata hivyo, wanaweza kukutana na mmoja wa hawa:

Bayern Munich, waliowachapa 2013 na 2014

Borussia Dortmund au Real Madrid

Benfica

Bayer Leverkusen

Porto au FC Copenhagen

OJuventus, Seville au Lyon

Kieran Gibbs pia aling'aa mechi hiyo

Watakaofuzu hatua ya Muondoano

Kundi A: PSG na Arsenal, Europa League (EL) - Ludogorets

Kundi B: Benfica na Napoli, EL - Besiktas

Kundi C: Barcelona na Manchester City, EL - Borussia Monchengladbach

Kundi D: Atletico Madrid na Bayern Munich, EL - FC Rostov

Kundi E: Monaco na Bayer Leverkusen

Kundi F: Borussia Dortmund na Real Madrid

Kundi G: Leicester na mmoja kati ya Porto na FC Copenhagen

Kundi H: Juventus na mmoja kati ya Sevilla na Lyon
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT