Aliyegombea urais CCM aomba kazi kwa JPM | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumatatu, 5 Desemba 2016

Aliyegombea urais CCM aomba kazi kwa JPM

Morogoro. Aliyekuwa mgombea urais kwenye mchakato wa CCM, akiwa mwanafuzi wa Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Umma katika Chuo Kikuu Muzumbe, Maliki Malupu amehitimu huku akisema yupo tayari kuitumikia Serikali iwapo Rais John Magufuli ataona ni muhimu kufanya naye kazi.

Malupu alisema kwa kiwango cha elimu alichofikia, ana uwezo mzuri wa kuitumikia Serikali kwa ufanisi zaidi na kuleta tija.

“Niseme tu naridhishwa na utendaji wa Rais (John) Magufuli, ingawa kuna maeneo machache yanatakiwa kurekebishwa hasa kwenye usimamizi mzima wa utoaji mikopo ya elimu ya juu,” alisema Malupu.

Alisema kazi ya utoaji mikopo halina utaratibu mzuri, kwani wapo wanafunzi wamepata lakini hawajapata chuo ilhali kuna waliopata vyuo na mkopo hawakupata.

Alisema kuna umuhimu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kusubiri kwanza udahili ukamilike ili utoaji mikopo ufuate.

“Haiwezekani bodi vya mikopo kuendelea na uteuzi wanafunzi wenye sifa ya kupata mkopo, huku Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ikiwa haijakamilisha udahili, hali hii inasababisha mgongano vyuoni,” alisema.

Malupu alisema hali ya uchumi kwa wanafunzi waliopo vyuoni siyo nzuri, jambo linaloweza kuhatarisha hatima yao kwa masomo iwapo Serikali haitachukua hatua za kuwanusuru.

Hivi karibuni HESLB ilisema tayari mikopo imetolewa kwa zaidi ya wanafunzi 26,000 na kwamba, kazi hiyo inaendelea. Akizungumza na gazeti hili mwaka jana wakati wa harakati zake, Malupu alisema iwapo angepitishwa na CCM angefanyia marekebisho utaratibu wa kumpima mhitimu wa sekondari kwa viwango vya GPA, kwani ulikuwa unawaathiri wanafunzi kisaikolojia.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT