Wayne Rooney ameweka rekodi ya kufunga magoli mengi ndani ya Manchester
United kwenye michuano ya Ulaya wakati wakitoa kichapo cha magoli 4-0
mbele ya Feyenoord na kuendelea kuweka matumaini ya kusonga mbele kwenye
michuano ya Europa League.
Nahodha huyo wa mashetani wekundu alifunga bao lake la 39 kwenye
michuano ya Ulaya ndani ya klabu yake wakati akiunganisha pasi ya Zlatan
Ibrahimovic na kuwaacha wachezaji wa Feyenoord wakilaumu kuwa mfungaji
alikuwa kwenye eneo la offside.
Rooney akatengeneza bao la pili ambalo lilifungwa na Juan Mata.
Baadaye golikipa wa zamani wa Liverpool alijifunga wakati akiwa katika
harakati za kuokoa krosi ya Ibrahimovic kabla ya Jesse Lingard kufunga
biashara dakika majeruhi na kumpa Jose Mourinho ushindi mkubwa akiwa
kama bosi wa United.
Sare au ushindi wa ugenini dhidi ya Zorya Luhansk kwenye mchezo wa
mwisho wa Kundi A siku ya Alhamisi Disemba 8, itaifanya United kufuzu
hadi hatua ya 32 bora.
Kipigo hiki ndio kikubwa kwa Feyenoord kwenye Uefa Cup/Europa League.
Walipoteza 5-1 dhidi ya Borussia Monchengladbach mwaka 1986.
Juan Mata amefunga mfululizo kwenye mechi za United kwa mara ya kwanza tangu Septemba 2015.
United walipiga mashuti 12 yaliyolenga goli (shots on target) dhidi ya
Feyenoord, mashuti yao mengi zaidi ndani ya mchezo mmoja kwenye michuano
yote msimu huu.
Feyenoord, wameshinda mechi moja tu kati ya mechi zao saba zilizopita walizocheza England kwenye michuano ya Ulaya (D2 L4).
United hawajapoteza mechi 14 za mashindano ya Ulaya kwenye uwanja wa Old
Trafford (pamoja na mechi za kufuzu), wameshinda mechi zote tatu za
hatua ya makundi msimu huu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT