Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limekiri kuwepo kwa changamoto
mbalimbali zikiwemo ucheleweshwaji wa ndege wakati wa kutoa huduma
katika maeneo ambayo yalipaswa kuhudumiwa.
Moja kati ya ndege mpya zinazotumiwa na ATCL |
Akizungumzia changamoto hizo, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo,
Mhandisi Emmanuel Korosso, amekiri kuwepo kwa changamoto ya marubani
ikizingatiwa mpaka sasa shirika hilo linatarajiwa kumaliza mafunzo ya
marubani 13 katikati ya mwezi Desemba.
Amesema kuhusu wafanyakazi, bodi yake imeagiza menejimenti ya shirika
hilo kusimamia kusimamisha kwa muda mktaba wa hiari ambao unatoa mwanya
kwa wafanyakazi kutumia vibaya ruhusa za matumizi ya tiketi za bure.
Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Mhandisi Emmanuel Korosso (Katikati) akizungumza na wanahabari leo.
Aidha, Bodi imemuagiza Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo kutangaza mara moja
nafasi zote za wakurugenzi na pia nafasi za mameneja zilizo wazi kwa
kufuata muundo wa muda uliopitishwa na bodi huku ikiwaondoa katika
nafasi zao wakurugenzi wote ispokuwa Mkurugenzi Mtendaji kutokana na
utendaji dhaifu pamoja na kutokuwa na sifa stahiki za elimu za kushika
nafasi walizonazo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT