Akizungumza na wakuu wa idara mbali mbali katika manispaa ya Kinondoni ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani humo makonda amedai kuwabaini wenyeviti na watendaji pamoja na wajumbe wa mitaa ndio vinara wa matumizi mabaya ya ofisi zao na kuchangia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.
Makonda ameendelea na ziara yake mkoani dar es salaa, huku akikumbana na vilio mbalimbali kutoka kwa wananchi dhidi ya watendaji wa serikali, wakiwemo nwenyeviti hao ambao wanatumia madaraka yao vibaya.
Aidha amesema kuna mpango maalum wa kuwapunguza watumishi ktk halmashauri za jiji la dsm wasiowajibika,huku pia akitaja idara ya ujenzi ktk manispaa ya kinondoni kuwa kinara ktk ubadhilifu na matumizi mabaya ya fedha za ujenzi wa barabara chini ya viwango.
Wakati huo huo mkuu wa mkoa wa dsm,mkuu wa wilaya ya kinondoni pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wametembelea tandale uwanja wa fisi kujionea hali ilivyo katika eneo hilo lililojipatia umaarufu kwa wadada kuuza miili yao, na hivyo kuagiza kwamba taratibu zinaandaliwa ili kuzibomoa nyumba hizo na kuunda viwanda vidogovidogo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT