Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema wamekubaliana na Rais wa Zambia Edgar Lungu katika kubadilisha sheria ya kumpata Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli la Tazara ili kusaidia kumpata mtendaji mwenye weledi.
Jukumu kubwa la Mtendaji huo itakuwa ni kuinua uwezo wa shirika hilo katika kukuza uchumi wa mataifa hayo mawili.
Rais Dkt. Magufuli amebainisha hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na Rais wa Zambia aliyekuja nchini ambapo amesema TAZARA haifanyi kazi vizuri kutokana na uongozi ambao umezorotesha uzalishaji.
Amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 1976 lilipoanzishwa shirika hilo lilikuwa na uwezo wa kusafirisha tani milioni 5 na sasa imeshuka hadi kufikia tani 128,000 kutokana na kuwepo kwa matatizo yasiyoisha yakiwemo migogoro ya wafanyakazi.
Rais Dkt. Magufuli ametaja sehemu ya mazungumzo yao kuwa ni pamoja na kuendeleza ushirikiano wa bomba la mafuta, ushirikiano katika ukuzaji wa uchumi, ujenzi wa kituo cha pamoja cha usafirishaji, ushirikiano ikiwemo kuunganisha kwa gesi ya Ethanol na Uunganishaji wa umeme baina ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Rais wa Zambia Edgar Lungu amesema wataendeleza ushirikiano baina ya nchi yake na Tanzania pamoja na kusifu utendaji wa Rais Dkt. Magufuli katika kuinua uchumi wa nchi na kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT